MKURUGENZI KAYOMBO AKUSANYA MILIONI 150 KWA MWEZI KATIKA SOKO LA NDIZI-MABIBO ILIHALI AWALI ZILIKUSANYWA MILIONI 10 KWA MWEZI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John lipesi Kayombo akizungumza na wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko ...


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John lipesi Kayombo akizungumza na wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifatilia kwa makini mkutano
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John lipesi Kayombo akitafakari kwa makini changamoto mbalimbali za wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa ziara ya kikazi katika soko la Ndizi-Mabibo
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo wakifatilia mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika katika Soko la Ndizi-Mabibo Jijini Dra es salaam
Wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifurahi mara baada ya kuambiwa wataendelea na shughuli zao katika soko hilo.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo amebaini ubadhirifu wa kiasi kikubwa cha pesa zinazofikia shilingi milioni tisini kila mwezi, unaofanywa na kikundi kinachojiita Majimoto kinachodai kupewa jukumu la kukusanya mapato katika soko la matunda la Mabibo kwa niaba ya mmiliki wa eneo hilo ambaye ni Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.

Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa ubadhirifu huo umebainika baada ya Halmashauri ya Manispaa kuchukua jukumu la kusimamia kwa muda ukusanyaji mapato katika soko hilo ambapo makusanyo yamepanda kutoka shilingi milioni saba zilizokuwa zinakusanywa hapo awali hadi zaidi ya shilingi milioni mia moja.

Kayombo amesema hayo wakati wa ziara ya ghafla iliyofanyika sokoni hapo na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kwa ushirikiano wa pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo sambamba na watendaji wote katika Manispaa hiyo,

Ziara hiyo imejili mara baada ya uongozi wa kiwanda cha Urafiki kutaka kuwaondoa kwa nguvu wafanyabiashara na kulifunga eneo hilo kwa kujenga uzio utakaozuia ufanyaji wa biashara.

Mkurugenzi amejibu hapo hapo agizo la Mkuu wa Wilaya Mhe Makori lilomtaka kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hao kwa kuwaagiza Afisa Afya na Mazingira wa Manispaa ya Ubungo kufuatilia malalamiko yaliyotolewa na wananchi katika mkutano huo kuhusu kiwanda cha nguo cha Urafiki ambacho kinalalamikiwa na wananchi kwa kuathiri afya zao kutokana na Moshi unaotoka kiwandani hapo.

Aidha mbele ya umati wa wafanyabiashara na wananchi katika mkutano huo Mkurugenzi Kayombo amemuagiza Kaimu Injinia wa Manispaa ya Ubungo kusambaza kifusi cha mawe kilichomwagwa sokono hapo kwa ajili ya kuzuia mlundikano wa maji.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa hivyo ameeleza dhamira yake ya kukusanya mapato ya Zaidi ya shilingi milioni 150 kwa mwezi katika soko la Ndizi-Mabibo na tayari mirija na mianya yote ya rushwa amefanikiwa kuiziba kwa kiasi kikubwa.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKURUGENZI KAYOMBO AKUSANYA MILIONI 150 KWA MWEZI KATIKA SOKO LA NDIZI-MABIBO ILIHALI AWALI ZILIKUSANYWA MILIONI 10 KWA MWEZI
MKURUGENZI KAYOMBO AKUSANYA MILIONI 150 KWA MWEZI KATIKA SOKO LA NDIZI-MABIBO ILIHALI AWALI ZILIKUSANYWA MILIONI 10 KWA MWEZI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghB2xfgt-MIbs95a9HTiIow1gOHyfN4lahwsFVEQ5j75WHeyLJXcNImGp5yxu5WhMOjE46m0DkNQZmhfNCeN_ZfTX7gmejYNENKNH6qGJeboBzqH6uM8L4qQSa6GVn58-xgPbMDXjQIQk/s640/1+%25282%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghB2xfgt-MIbs95a9HTiIow1gOHyfN4lahwsFVEQ5j75WHeyLJXcNImGp5yxu5WhMOjE46m0DkNQZmhfNCeN_ZfTX7gmejYNENKNH6qGJeboBzqH6uM8L4qQSa6GVn58-xgPbMDXjQIQk/s72-c/1+%25282%2529.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mkurugenzi-kayombo-akusanya-milioni-150.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mkurugenzi-kayombo-akusanya-milioni-150.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy