MBUNGE WA KIBAHA MJINI SYLVESTRY KOKA AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA 'KUTUMBUA JIPU' LA UUZAJI WA KIWANJA CHA ZAHANATI. ASHIRIKI USAFI WA ENEO LA KUJENGWA ZAHANATI

 Na Ripota wa Mafoto Blog, Kibaha MBUNGE wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka (kulia) na Diwani wa Kata ya Sofu, Yusuf Mbonde, wakishiriki...


 Na Ripota wa Mafoto Blog, Kibaha

MBUNGE wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka (kulia) na Diwani wa Kata ya Sofu, Yusuf Mbonde, wakishirikiana na wananchi wa kata hiyo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kusafisha eneo lililo na majani kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa Zahanati. Mhe. Mbunge leo asubuhi alifanya ziara ya kushitukiza katika eneo hilo baada ya kupata tetesi kuwa eneo hilo limeuzwa.

Aidha imeelezwa kuwa tetesi za kuuzwa kwa eneo hilo zilimfikia Diwani wa Kata hiyo, Bw.Mbonde, aliyeamua kumfuata Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kibaha, Jenifer Ommolo, ambaye 'eti' alikiri kuwa jambo hilo nalitambua na kumwahidi kuwa wangepewa eneo mbadala wa hilo, jambo ambalo Diwani hakukubariana nalo na kuamua kulifikisha kwa Mhe.Mbunge wake.

Mbunge huyo, alifika eneo hilo na kukutana na wapiga kura wake na kuamua kushiriki nao zoezi la kusafisha baada ya baadhi ya wananchi kukumbwa na hofu wakidai kuwa eneo hilo lilibadilishwa lengo la matumizi kwa kumgawia mtu aliyejulikana kwa jina la Mchome, ili kuliendeleza, ambaye pia hadi Mbunge anafika leo alikuwa bado hajaanza ujenzi wa aina yeyote.
Imeelezwa kuwa eneo hilo baada ya kutolewa kwa ajili ya kujengwa Zahanati ambayo kwa kiasi kikubwa ilitakiwa kujengwa kwa ushirikiano mkubwa na wananchi ambao wengi wao walipigwa na butwaa na kurudi nyuma baada ya kusikia eneo hilo amegaiwa Mchome, aliyetakiwa kuliendeleza.
Baada ya Mbunge Koka kuwasili eneo hilo hii leo asubuhi, wananchi wajitokeza na kuonyesha ushirikiano huo kwa kushirikiana na viongozi wao, na baadaye kubaki na matumaini ya kuona kinajengwa kile walichokikusudia baada ya Mbunge kutoa tamko kwa kusema eneo hilo linatakiwa kujengwa Zahanati ya wananchi na si kitu kingine.
 Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza na wananchi wa Kata ya Sofu Wilayani Kibaha, wakati wa zoezi la kufyeka na kusafisha eneo la kujenga Zahanati,ambapo alilaani kitendo hicho cha uuzwaji wa eneo la wananchi alichokiita cha kitapeli.
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao, baada ya zoezi hilo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBUNGE WA KIBAHA MJINI SYLVESTRY KOKA AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA 'KUTUMBUA JIPU' LA UUZAJI WA KIWANJA CHA ZAHANATI. ASHIRIKI USAFI WA ENEO LA KUJENGWA ZAHANATI
MBUNGE WA KIBAHA MJINI SYLVESTRY KOKA AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA 'KUTUMBUA JIPU' LA UUZAJI WA KIWANJA CHA ZAHANATI. ASHIRIKI USAFI WA ENEO LA KUJENGWA ZAHANATI
https://1.bp.blogspot.com/-5oDZA9Vk2yA/WWEfaTR7IaI/AAAAAAADBGQ/6wHvBLH6JAAR3R9FiCYl75AuGctvnvwzACLcBGAs/s640/5.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-5oDZA9Vk2yA/WWEfaTR7IaI/AAAAAAADBGQ/6wHvBLH6JAAR3R9FiCYl75AuGctvnvwzACLcBGAs/s72-c/5.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mbunge-wa-kibaha-mjini-sylvestry-koka.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mbunge-wa-kibaha-mjini-sylvestry-koka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy