MANISPAA YA UBUNGO YAANZISHA REJESTA YA WAKAZI KWA KILA MTAA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananch...


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali muda mchache mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM  Julai 5, 2017.
 

 Mfano wa Fomu ya huduma kwa mwananchi (Fomu ya malalamiko)

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika Manispaa ya Ubungo.Leo June 5, 2017

 Kitabu cha Kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika ofisi za serikali

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika Manispaa ya Ubungo Julai 5, 2017

 Mfano wa Fomu ya Rejista ya Wakazi katika kila Mtaa


Ili kupunguza uhalifu katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam imebainika kuwa ni vyema kuwatambua wananchi wote na mahali wanapoishi ikiwemo kubaini wageni wote wanaowasili katika Manispaa ya Ubungo ikiwa ni pamoja na mahali wanapofikia.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba Chama Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa  kumekuwa na uhalifu kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali Katika Manispaa hiyo jambo ambalo limetafutiwa muarobaini kwa kuanzishwa daftari la wakazi litakalobainisha wakazi wote ili kukitokea uhalifu iwe rahisi kuwabaini wahalifu hao.
Kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya Wakazi wa Mtaa ni agizo lililotolewa hivi karibuni na MKUU wa Wilaya ya Temeke Mhe Felix Lyaviva kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa za Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni na Ubungo wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda katika ufunguzi wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili kuwaelimisha watumiaji wa Intaneti wapatao milioni 20 sambamba na watumiaji wa simu za mikononi wapatao milioni 40 kuwa na matumizi bora ya simu za mikononi na mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amesema kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya wakazi wa Mtaa pia kutakuwa na Fomu ya Rufaa ya Malalamiko katika kila Mtaa sambamba na kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali.

Tayari vitabu hivyo vyote vimeanza kugawanywa katika kila Mtaa ili kuanza utekelezaji wa zoezi hilo haraka iwezekanavyo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO 
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MANISPAA YA UBUNGO YAANZISHA REJESTA YA WAKAZI KWA KILA MTAA
MANISPAA YA UBUNGO YAANZISHA REJESTA YA WAKAZI KWA KILA MTAA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhym7Vq9xt2YALbCzRaJbgpGDapfoUFOoELdrjmhGbT8EhrU6TYk80PZp1um4vZ8DJtd0830Q4Q3V96bbzPFmtdfuh_v8EFn0_ELUr45WKn-mee7PQKwlMdb0gyL_OiTTtgZGx6CpsRZP0/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhym7Vq9xt2YALbCzRaJbgpGDapfoUFOoELdrjmhGbT8EhrU6TYk80PZp1um4vZ8DJtd0830Q4Q3V96bbzPFmtdfuh_v8EFn0_ELUr45WKn-mee7PQKwlMdb0gyL_OiTTtgZGx6CpsRZP0/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/manispaa-ya-ubungo-yaanzisha-rejesta-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/manispaa-ya-ubungo-yaanzisha-rejesta-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy