MAKAMU WA RAIS, SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES

Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ...


Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo.
Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA

Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


Abraham Ntambara.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.

“Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo
mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais. Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu
mengine.
Aliahidi kuifanyia changamoto iliyotajwa ya matumizi ya
mitandao ya kijamii ambapo alisema atalisimamia hilo kwani ni vizuri kutumia mitandao hiyo kwa kuzingatia maadili kutokana na hivi sasa watu kuitumia vibaya.
Pia alitoa pendekezo la chama hicho kubuni miradi mingine
ambayo inaweza kuwaingizia fedha ili kuacha kutegemea wahisani.

Mama Salma Kikwete wakati akimuachia jukumu hilo la kukilea
chama hicho alimkabidhi vitu vitatu ambavyo ni Bendera ya Taifa ya chama,
Katiba na mpango mkakati wa chama na kumvalisha Skafu ya chama kama ishara ya
kukabidhiwa rasmi kijiti hicho.

Aidha alisema kuwa chama kimekuwa na mafanikio makubwa ikiwa
ni pamoja na kuweza kuongeza wanachama kutoka 97,143 hadi kufikia wanachama 100,008 mwaka huu.
Aliongeza kwamba wanatarajia mwezi Septemba kuapisha
wanachama 300 katika mkoa huku akieleza kwamba tayari wamekwisha sajili zaidi ya wanachama 2000 katika mkoa wa lindi.


Kikundi cha sanaa cha Ilala kikitumbuiza 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye pia ni Kamishna wa TGGA, Sophia Mjema akimlaki aliyekuwa Mlezi wa TGGA Mama Salma Kikwete

Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi

Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba

Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA




Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides




Samia akipata maelezo  kutoka kwa Mkufunzi wa Girl Guides Ruth kuhusu kazi mbalimbali za TGGA

Samia na Salma Kikwete wakilakiwa na Girl Guides

Brass Band ya Polisi ikiongoza wimbo wa Taifa

Viongozi mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo

Baadhi ya makamishna wa TGGA wakiwa katika sherehe hiyo

Mwenyekiti wa TGGA Profesa Martha Qorro akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa

Kamishna Mkuu wa TGGA Symphorosa Hangi akisema neno la utangulizi pamoja na kutambulisha  wageni waalikwa 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Abdalah akihutubia wakati wa sherehe hiyo

Aliyekuwa Mlezi wa TGGA, Mama Salma Kikwete akihutubia kabla ya kumkabidhi ulezi Makamu wa Rais Samia

Ni furaha iliyoje

Salma Kikwete akimvisha skavu Mlezi mpya wa TGGA, Samia Suluhu Hassan

Wasanii wa Shule ya Msingi Umoja wakitumbuiza wakati wa sherehe hiyo
Ni wakati wa furaha
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema na Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdalah wakichenza ngoma


Mama Samia akimtunza fedha kiongozi wa kikundi cha Umoja kwa kucheza vizuri

Kamishna Mkuu wa TGGA akimkabidhi zawadi ya saa  Mlezi mstaafu wa TGGA, Mama Salma Kikwete

Mama Salma akionesha Saa hiyo




Girl Guides wakighani shairi maalumu

Baadhi ya makamishna wakiimba wimbo maalumu

NI FURAHA TELE

Viongozi na makamishna wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi mpya wa TGGA, Samia

Mlezi mpya, Mama Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na makamishna wa mikoa

Mama Samia na Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA

Girl Guides wakiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Mlezi mpya, Samia


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS, SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES
MAKAMU WA RAIS, SAMIA AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES
https://1.bp.blogspot.com/-Rm9WUl6Ul5M/WWYhZfwktsI/AAAAAAABFyI/D6vup7_MaAca5BeXb9Ue3vvefPFFVo8AACLcBGAs/s640/IMG_9724.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-Rm9WUl6Ul5M/WWYhZfwktsI/AAAAAAABFyI/D6vup7_MaAca5BeXb9Ue3vvefPFFVo8AACLcBGAs/s72-c/IMG_9724.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-samia-amrithi-mama-salma.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-samia-amrithi-mama-salma.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy