MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA AONGOZA WATANZANIA KUSHUHUDIA MECH YA EVERTON NA GOR MAHIA

Na Shamimu Nyaki-WHUSM. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan jana ameongoza Watanzania na w...



Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan jana ameongoza Watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Everton ya Uingereza na Gor Mahia kutoka Kenya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulihudhuriwa na Viongozi wa mbalimbali wa Kitaifa wakiwemo Marais wastaafu Mhe. Alhaj Alli Hassan Mwinyi na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Balozi wa Uingereza nchini Bibi. Sarah Coker pamoja na viongozi wengine.
Katika mchezo huo uliochezwa zaidi ya dakika 90 timu ya Everton iliibuka mshindi wa magoli mawili dhidi ya goli moja la Gor Mahia. Goli la kwanza la Everton likifungwa na nyota wake Wayne Rooney katika dakika ya 34 kipindi cha kwanza na baadaye timu ya Gor Mahia iliweza kusawazisha katika dakika ya 37 kupitia mchezaji wake Tuyisenge Jacquer.
Katika Kipindi cha pili, timu zote zililirudi kwa kasi zikionyesha mbinu mbalimbali za kuukabili mpira na dakika ya 71 Everton ilijipatia goli la pili kupitia   mchezaji wake   Kierdin Dowell na hivyo kuibuka washindi   dhidi ya Gor Mahia kwa magoli 2-1.
Mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki yenye lengo la kuimarisha timu zao pamoja na mahusiano katika sekta ya michezo katika nchi za Uingereza na Afrika Mashariki iliyoandaliwa na Kampuni ya SportPesa ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa ligi kwa mwaka 2017/2018 kwa mataifa mbalimbali duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Everton ya England na Gor Mahia ya Kenya  kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya timu hizo mbili jana katika uwanja wa Taifa Jijini  Dar es Salaam pembeni yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto)      pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni  Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) wakifuatilia mechi kati ya Everton ya England na Gor Mahia ya Kenya jana katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Gor Mahia ya Kenya wakishangilia baada ya kupata bao lililofungwa na mchezaji Tusiyege Jacqer kwenye mechi yao dhidi ya Everton ya England jana  katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Everton ya England na Gor Mahia ya Kenya  wakiwa uwanjani  jana Jijini Dar es Salaam.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA AONGOZA WATANZANIA KUSHUHUDIA MECH YA EVERTON NA GOR MAHIA
MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA AONGOZA WATANZANIA KUSHUHUDIA MECH YA EVERTON NA GOR MAHIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzkH3Zobk8wVjqJEa3qAOLleGqWpDCMebU4iS41pHOz5nl8xXX_iJlxMktpycsb4HgKl2q6F0h_FE7ZW8MZyEuEod2oIGkv2UDo2Y2zrKWvshQ3KEotYjlKayPV6orT501HQFFAIL7_JE/s640/pix+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzkH3Zobk8wVjqJEa3qAOLleGqWpDCMebU4iS41pHOz5nl8xXX_iJlxMktpycsb4HgKl2q6F0h_FE7ZW8MZyEuEod2oIGkv2UDo2Y2zrKWvshQ3KEotYjlKayPV6orT501HQFFAIL7_JE/s72-c/pix+1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-mhe-samia-aongoza.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-mhe-samia-aongoza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy