MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira...


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira bora yatakayosaidia mamia ya wananchi nchini wanapata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi mjini na vijijini.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Makampuni ya Simu Duniani (GSMA MOBILE 360) Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassana amesema anaimani kuwa wadau hao wa makampuni ya simu watajadili kwa kina namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na kuweka mipango mizuri ya kufikia wananchi wengi zaidi hasa maeneo vijijini ambayo baadhi ya maeneo hayafikiki kutokana na uduni wa miundombinu.

“Ningependa kusema kwamba Tanzania inakubali sana ushirikiano na GSMA na tunatamani kupanua ushirikiano wetu na uwezeshaji kwa Watu wetu kwa njia ya sekta ya simu ili kufikia utekelezaji wa ajenda za Maendeleo endelevu ya Umoja wa Afrika AU na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020”.Amesisitiza Makamu wa Rais.

Ameleeza kuwa kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi kadhaa Kusini mwa Bara la Afrika ambayo inafanya vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia simu za mkononi na kusema kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na akaunti za benki hivyo huduma hiyo huwasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kutuma fedha kwa urahisi.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa zaidi kwa huduma za kisasa za kimtandao ili wananchi waweze kunufaika zaidi kwa njia hiyo katika sekta za elimu,afya, kilimo, biashara na masuala ya kijinsia.

Amewahakikishia wadau hao wa makampuni ya simu kuwa Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarisha huduma zake kwa njia ya kisasa kwa wananchi.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya itaendelea kujifunza kutoka nchi zingine ambazo zimefanya vizuri katika sekta ya mawasiliano ili taifa na wananchi wake liweze kunufaika ipasavyo na huduma hizo kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema akizungumza katika mkutano huo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Makampuni ya Mawasiliano ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa.


Imetolewa na 
Ofisi ya Makamu wa Rais wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam.
11-Julai-2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.
 
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM
https://2.bp.blogspot.com/-s8m_veNTJKo/WWTlDqqxFLI/AAAAAAAJrx0/oymc9Wg1g2o2UsypPqDRFxFP9HXvIr8NwCLcBGAs/s640/1.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-s8m_veNTJKo/WWTlDqqxFLI/AAAAAAAJrx0/oymc9Wg1g2o2UsypPqDRFxFP9HXvIr8NwCLcBGAs/s72-c/1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-afungua-mkutano-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy