F MABADILIKO MAKAMANDA WA POLISI: ACP MULIRO ALETWA KINONDONI | RobertOkanda

Tuesday, July 18, 2017

MABADILIKO MAKAMANDA WA POLISI: ACP MULIRO ALETWA KINONDONI


 Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP),  Muliro Jumanne Muliro.
  MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP), Simon Nyankoro Sirro, (pichani), amefanya mabadiliko madogo kwenye Jeshi hilo leo Julai 18, 2017 ambapo, amemuhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Suzan Kaganda, na kumpeleka Makao Makuu ya Jeshi hilo ambako atahudumu kama, Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia. Nafasi yake imechukuliwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP),  Muliro Jumanne Muliro.
Habari zaidi nenda hapo chini.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Suzan Kaganda

0 comments:

Post a Comment