Na Paschal Dotto - MAELEZO Kampuni ya “Kuja Na Kushoka Tools Manufactures Group” imeunga mkono jitihada za serikali utunzaji mazin...
Na Paschal Dotto -
MAELEZO
Kampuni ya “Kuja Na
Kushoka Tools Manufactures Group” imeunga
mkono jitihada za serikali utunzaji mazingiza na kuwa na uchumi wa kati kupitia
viwanda kwa kubuni mashine inayotengeneza nishati ya mkaa mbadala kwa kutumia mabaki
ya mazao na takataka badala ya kukata miti.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dare es salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Leonard
Kushoka amesema kuwa ugunduzi huo
utarahisisha matumizi ya nishati hiyo ambayo ni mkombozi kwa wananchi wa kipato
cha kati na chini.
“Teknolojia hii ni njia
mbadala na salama kwa mazingira kwani inatumia taka za aina zote pamoja na
mabaki ya mazao badala ya kukata miti, vilevile ni njia ya utunzaji wa
mazingira kutokana na takataka hizo kutumika katika kuzalisha mkaa kwa matumizi ya
nyumbani”. Alisema Kushoka.
Bw. Kushoka ameongeza kuwa
katika miji mikubwa kama Dar es salam,
Mwanza na Arusha matumizi ya nishati ya mkaa ni makubwa kutokana na kuwa na
idadi kubwa ya watu ikiwa jiji la Dar es
salam pekee matumizi ya mkaa yanafikia magunia 28,000 kwa siku sawa na asilimia
50 ya mkaa wote unaozalishwa nchini ikifuatiwa na Mwanza na Arusha.
Aidha Bw.Kushoka alisema
kuwa mashine hiyo yenye uwezo wa kuzalisha magunia 20 ya mkaa kwa siku inatumia
nishati ya mafuta ya dizeli au umeme kutegemea na matakwa ya mteja na inauzwa
kwa shilingi milioni 15.
Bw. Kushoka aliongeza
kuwa licha ya mashine hiyo kulinda mazingira pia inaongeza thamani ya mazao
kwani mabaki yote ya mazao yanatumiwa na mashine hiyo kuzalishia mkaa mbadala kama
malighafi.
Kampuni hii ilianzishwa
mwaka 2000 mkoani Tabora kwa lengo la kutunza mazingira kwa kutumia teknolojia ya
kisasa na inafanya kazi kw karibu na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) pamoja na
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
COMMENTS