F IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA MAGARI MANNE JIJINI DAR ES SALAAM | Okandablogs

Thursday, July 6, 2017

IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA MAGARI MANNE JIJINI DAR ES SALAAM1 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akisikiliza maelekezo ya jinsi inavyotumika moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval kutoka China, ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Kifaru, Mario Gaspari.Hafla hiyo imefanyika Julai 5, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa Polisi Oysterbay ijini Dar es Salaam.

unnamed
Mkuuwa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Meneja Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Haval kutroka China, Bw.Jianguo Liu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni juhudi zake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini.Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam

2
Mkuuwa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akikagua moja ya magari hayo.
3
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akitoa hotuba yake.
4
Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu, akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano ya magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ambapo aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu nchini.Kushoto aliyesimama ni mkalimani wa lugha ya Kichina. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
5
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akipita mbele ya magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu.Hafla hiyo imefanyika Julai 5, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
6
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro(wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu,(watatu kushoto),baada ya makabidhiano ya magari manne kutoka kwakampuni hiyo ikiwa ni mchango wao katika kulisaidia Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu nchini.Wengine ni viongozi wa juu wa jeshi na viongozi wa kampuni ya Haval kutoka China. Hafla hiyo imefanyika Julai 5, 2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

0 comments:

Post a Comment