HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI YAWEZESHA WATOTO KUSIKIA KWA MARA YA KWANZA

Watoto watano waliofanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa maalum  vya kusaidia kusikia (Cochlear ...

kifa1 kifa2Watoto watano waliofanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa maalum  vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant) leo wamewashiwa vifaa hivyo ili waweze kusikia kwa mara ya kwanza.
Zoezi hilo  limefanywa leo na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaam kutoka MEDEL .
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Edwin  Liyombo amesema Juni   5 na 6 mwaka huu watoto hao walifanyiwa upasuaji huo kwa mara ya kwanza na kuwekewa vifaa maalum kwa ajili ya kusikia (Internal complete) lakini leo wamekuja kuwekewa na  kuwashiwa  vifaa vya nje(External complete) ili waweze kusikia.
Kwa upande wake mtaalam wa vifaa vya usikivu Fayaz Jaffer amesema baada ya kuwekewa kifaa hivyo watoto hao wanapaswa kurudi kila baada ya wiki mbili kwa miezi mitatu na baada ya hapo  watarudi  wiki mbili kwa miezi sita ili kufanyiwa mazoezi.
‘’Baada ya hapo wanaanza kuwafanyia mazoezi ya kuongea ( speech therapy) ndani ya mwaka mmoja na kadiri umri unavyozidi kwenda watakuwa wameshaanza kusikia na kujifunza kuongea na kupelekwa kujifunza zaidi katika shule za kawaida na si shule maalum kama ilivyozoeleka” amesema mtaalam huyo.
Juni 7 mwaka huu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alizindua huduma ya upasuaji wa kupandikizaji wa vifaa vya usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , ambapo katika Hospitali za Umma Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo  na ya pili katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI YAWEZESHA WATOTO KUSIKIA KWA MARA YA KWANZA
HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI YAWEZESHA WATOTO KUSIKIA KWA MARA YA KWANZA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/07/kifa1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/hospitali-ya-taifa-ya-muhimbili.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/hospitali-ya-taifa-ya-muhimbili.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy