CRB YAWATAHADHRISHA WAKANDARASI DHIDI YA MATAPELI

BODI ya Usajili wa Wakandarasi Nchini (CRB), imewatahadharisha wananchi, watu  wenye miradi ya ujenzi pamoja na wakandarasi nchi...


BODI ya Usajili wa Wakandarasi Nchini (CRB), imewatahadharisha wananchi, watu  wenye miradi ya ujenzi pamoja na wakandarasi nchini kuwa makini na watu wanaotumia jina la bodi hiyo na kufanya utapeli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msajili wa bodi hiyo, Rhoben Nkori, bodi imewataka wananchi na wakandarasi wawe wanatoa taarifa katika ofisi za bodi za Makao Makuu Dar es Salaam na Kanda zake ili kuwakamata na kuwafikisha mahahani watu wa aina hiyo.

“CRB ina ofisi za kanda ambazo zinafanya kazi nchi nzima, kanda hizo ni Kanda ya mashariki – Dar es Salaam, Kanda ya kaskazini  Arusha, Kanda ya kusini Mbeya,  Kanda ya ziwa Mwanza

na Kanda ya kati  Dodoma, watumie ofisi hizi wasirubuniwe na matapeli,” alisema Nkori.

Aidha, alisema watumishi wa CRB wamekuwa wakienda kwenye ukaguzi wakiwa na vitambulisho vya bodi hiyo na vizibao vyenye nembo ya CRB vinayowatambulisha kuwa wanatoka bodi hiyo.

Alisema kuna watu ambao wamekuwa wakijiita wawakilishi wa Bodi hiyo na kufanya shughuli za bodi hiyo kwa njia ya utapeli na kuchukua rushwa kwa wakandarasi na wenye miradi.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa jana na  CRB, watu hao wamekuwa wakijitambumbulisha kama wawakilishi wa bodi hiyo ambao huwa wanakwenda kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi maeneo mbalimbali.

Alisema watu hao hutembelea sehemu zenye miradi na kuwatisha watu wanaofanya shughuli za ujenzi na kuwaomba rushwa ili wasiwashtaki wanapobaini kasoro kwenye miradi yao.

Aidha, alisema watu hao wamekuwa wakiwaandikia barua watu wenye miradi ya ujenzi wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua na bodi kwa kufanyakazi zao bila kuzingatia masharti ya ujenzi kama vile kuweka vibao vya kuonyesha mkandarasi anayejenga.

“Sisi CRB hatuwatambui watu hao na tunawaomba wananchi na watu wenye miradi ya ujenzi wawe makini na wakiwa na tatizo waende kwenye ofisi za kanda zetu ambazo tumezitaja kama kuna watu anahisi wanataka kumtapeli awasiliane na bodi ili tumkamate na kumfikisha mahakamani,” alisema

Gazeti hili lilifanikiwa kupata nakala ya barua yenye nembo ya CRB iliyoandikwa na mmoja wa matapeli hao kwenda kwa mmoja wa wateja akidai kutaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye mradi wake wa ujenzi unaoendelea.

 Kwenye barua hiyo kwenda kwa mteja tapeli huyo  aliandika hivi “ I need the following drawings, architectural drawing, structural drawing and Building permit and sign board.

“Hapo anamaanisha kuwa mteja huyo amuonyeshe mchoro wa jengo, kibali cha ujenzi na kibao ambacho kisheria kinapaswa kuwekwa sehemu ya ujenzi kikionyesha jina la mteja, mkandarasi, mhandisi mshauri na  mkandarasi”alisema

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: CRB YAWATAHADHRISHA WAKANDARASI DHIDI YA MATAPELI
CRB YAWATAHADHRISHA WAKANDARASI DHIDI YA MATAPELI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvVtHdHyLK1eSVL6_gO1Hp4uAd8c2wncrJYXpIOq6yRTFso5ea-cYbM1ifGBA2lWG70c-hbk0OHEGsQ5wcEbnNkV9gsu2m4An0QyaAgAE3Od5yMoYXlM9tby2IsBY7BiR9H0zSfumDigYc/s640/pix3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvVtHdHyLK1eSVL6_gO1Hp4uAd8c2wncrJYXpIOq6yRTFso5ea-cYbM1ifGBA2lWG70c-hbk0OHEGsQ5wcEbnNkV9gsu2m4An0QyaAgAE3Od5yMoYXlM9tby2IsBY7BiR9H0zSfumDigYc/s72-c/pix3.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/crb-yawatahadhrisha-wakandarasi-dhidi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/crb-yawatahadhrisha-wakandarasi-dhidi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy