BANK OF AFRICA YAKABIDHI RASMI MTAMBO WA UJENZI AINA YA GREDA KWA MTEJA WAKE

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Wasia Mushi akikabidhi mfano wa funguo kuashiria makabidhiano ya Greda kwa Mteja B...Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Wasia Mushi akikabidhi mfano wa funguo kuashiria makabidhiano ya Greda kwa Mteja Bw. T Hitesh Vishram ambae ni Project Supervisor wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Limited, Katikati ni meneja wa masoko, Utafiti na maendeleo wa Bank of Africa Tanzania, Muganyizi Bisheko.


BANK OF AFRICA hii leo imekabidhi rasmi mtambo wa ujenzi (Greda jipya aina ya JCB) lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kampuni ya Dezo Civil Contactors Limited, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo kandarasi ya ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi.

Makabidhiano ya mtambo huu ni sehemu ya mpango endelevu wa benki wa kununua na kukodisha mitambo (lease finance), ambayo inawawezesha wateja kujiongeza kiutendaji kwa kupata vifaa vya kisasa bila ya kulazimika kuwa na pesa taslimu za manunuzi ya vifaa hivyo.

Makubaliano haya ya ukodishaji wa mitambo yanaakisi katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii, madini, mafuta na gesi

BANK OF AFRICA imebaini huu ni mpango ambao una tija kubwa kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo, kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa biashara zao ambao utaongeza uzalishaji na faida kubwa. Mteja kupitia mpango huu anapewa fursa pana ya kufanya chaguo lake bila kikwazo chochote na bila ya uhitaji wa amana ya awali au dhamana nyingine. Marejesho ni malipo ya ukodishaji ya kila mwezi na mteja ana uwezo wa kuchagua kua mmiliki wa mali husika pindi ifikapo mwisho wa mkataba wa ukodishaji.

Benki humsaidia mteja kuhakiki chombo anachotaka kuingianacho mkataba kama kina ubora ili kuweza kuinua uchumi wake na uchumi wataifa kwa ujumla


BANK OF AFRICA ilianza shughuli zake Juni mwaka 2007, baada ya kuinunua Benki ya Euroafrican ambayo ilianza kazi Tanzania kutokea September 1995

BANK OF AFRICA inafanya kazi katika mtandao wa benki za biashara katika nchi 18 zikiwamo nchi za Benin, Burkina Faso, Burundi, Cote d”ivoire, Djibouti, DRC, Ethiopia, France, Ghana, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Rwanda, Senegal, Tanzania, Togo na Uganda

Kundi la Group BANK OF AFRICA lina makao makuu yake jijini Dakar, Senegal ikiwa na mtandao wa watu 500 wale wanaotoa huduma na sapoti kwa ofisi. Kuanzia mwaka 2010, Group BANK OF AFRICA ilimilikiwa kwa wingi wa hisa BMCE Bank, ambayo ni benki ya pili kwa ukubwa nchini Morocco.

BMCE Bank huleta mikakati mizito ya msaada wa uendeshaji katika kuunga mkono shughuli za BANK OF AFRICA Group, vilevile na muunganiko na ukaribu wa kufikia masoko ya kimataifa kutokana na uwepo wake katika nchi za Ulaya na Asia.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BANK OF AFRICA YAKABIDHI RASMI MTAMBO WA UJENZI AINA YA GREDA KWA MTEJA WAKE
BANK OF AFRICA YAKABIDHI RASMI MTAMBO WA UJENZI AINA YA GREDA KWA MTEJA WAKE
https://3.bp.blogspot.com/-CePGmGBUpwc/WWym6Md4xKI/AAAAAAAAFlE/X-FyuIZexSkGxJrbkha_c8tQ8t2Ae58FwCLcBGAs/s640/X2.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-CePGmGBUpwc/WWym6Md4xKI/AAAAAAAAFlE/X-FyuIZexSkGxJrbkha_c8tQ8t2Ae58FwCLcBGAs/s72-c/X2.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/bank-of-africa-yakabidhi-rasmi-mtambo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/bank-of-africa-yakabidhi-rasmi-mtambo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy