BALOZI ADADI: AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANSI

Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza imepatiwa na Wi...



Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi

Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza
imepatiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule
zote za sekondari wilayani humo juzi wakati alipokwenda kukabidhi kulia
ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Luiza Mlelwa kushoto ni Afisa Elimu
Sekondari wilaya hiyo Julitha Akko
Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari.

Muheza High School, Luqman Mustapha akimueleza Mbunge wa Jimbo la
Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu juzi namna wanayotumia vifaa vya maabara
walivyopatiwa wakati alipokabidhi vifaa vya maabara  kwa shule za
sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa nchini

MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa nchini.


Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara
kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya
ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa
chini.

Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika shule 7 kati ya 24

wilayani humo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuweza kufikia malengo yao
ya kufanya vizuri katika masomo yao katika hafla hiyo iliyofanyika
shule ya sekondari ya Muheza.

“Jambo hilo ni nzuri na hasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali
la kutaka vifaa hivyo vikabidhiwe katika shule ambazo zitakuwa
zimekamilisha ujenzi wa maabara na vitaweza kuwapa mwanga mzuri kusoma
kwa bidii “Alisema.


Alisema ni jambo la ajabu iwapo vifaa ambazo vimekabidhiwa vitatumika
vibaya kitendo ambacho kitakwamisha juhudi za serikali za kutaka
wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kuendana na
sera ya viwanda.


“ Vifaa hivi ambavyo mmekabidhiwa leo hii vinagharama kubwa hivyo
niwaombe ndugu zangu mhakikishe mnavitunza ili viweze kutumika katika
matumizi yaliyokusudiwa lakini pia niwatake wanafunzi mhakikishe mnasoma
kwa bidii “Alisema



Mbunge huyo alisema lipo tatizo la kubwa la kutokuwepo vifaa vya maabara
katika shule nyingi za sekondari hapa nchini jambo ambalo limeanza
kupatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya elimu
ili kuona namna ya kulimaliza.



Awali akizungumza katika hafla hiyo, Afisa elimu sekondari wilaya Muheza
Julitha Akko amewaagiza walimu wakuu wa shule za sekondari zilizopatiwa
vifaa hivyo kuacha tabia ya kufungia ndani ya makabati na badala yake
vitumike kama ilivyokusudiwa.


Aidha alisema kuwa lazima kuwekwe utaratibu wa namna ya kuvitunza vifaa
hivyo na kuagiza visitumike kinyume na makusudio yake na kuwataka
wanafunzi waelekeze nguvu zao kwenye masomo ili kuongeza wataalamu wengi.


Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Muheza (Muheza high school)
Alex Birumo alisema yapo mategemeo makubwa ya kuongeza ufaulu hasa kwa
masomo ya sayansi kutokana na kupatikana kwa vifaa hivyo ambavyo
wanafunzi walikosa fursa kwa miaka mingi kujifunza kwa vitendo.


“Shule yetu hii ni ya masomo ya sayansi ya michepuo ya PCB NA CBG na ni
ya kidato cha tano na sita unapokuwa na wanafunzi zaidi ya 150
unawafundisha bila ya vifaa vya maabara kiukweli mafunzo yetu kwa
wanafunzi hao yahakuwa na tija”Alisema
(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI ADADI: AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANSI
BALOZI ADADI: AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANSI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgFamtTwUneHpceztPGo-9zOuQX55IO8JBhz3g9AZxc5cEWxRP8bExqmfRPbNm-Ac47SPtcZF7ONEa-jrP_xhN4SmsxyFpFinMIaPUnfa5V7uOB9cELvjGvYtInsda_Z5pndZPLxiMfPrDw/s640/1%25281%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgFamtTwUneHpceztPGo-9zOuQX55IO8JBhz3g9AZxc5cEWxRP8bExqmfRPbNm-Ac47SPtcZF7ONEa-jrP_xhN4SmsxyFpFinMIaPUnfa5V7uOB9cELvjGvYtInsda_Z5pndZPLxiMfPrDw/s72-c/1%25281%2529.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/balozi-adadi-awataka-wanafunzi-wilayani.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/balozi-adadi-awataka-wanafunzi-wilayani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy