F YAMETIMIA: VIDEO MABOSI WA IPTL, HARBINDA SIGH SETHI NA JAMES RUGEMALILA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA UHUJUMU UCHUMI | Okandablogs

Monday, June 19, 2017

YAMETIMIA: VIDEO MABOSI WA IPTL, HARBINDA SIGH SETHI NA JAMES RUGEMALILA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA UHUJUMU UCHUMI


kamc2
Harbinder Singh Sethi na James Rugemalila wakiwa wamechuchumaishwa na polisi tayari kupelekwa chumba cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2017. Watuhumiwa wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya uhujumu uchumi.TAKUKURU imesema inawashikilia Harbinder Singh Sethi na James Rugemalila kwa makosa ya uhujumu uchumi. Wanapelekwa kwenye mahakama ya Kisutu na baadae watapelekwa Mahakama ya Maalumu ya kifisadi. “Ndugu wanahabari, leo tumekutana tena mchana huu, ili kuwapeni taarifa za mapambano yetu dhidi ya rushwa na Ufisadi nchini. Na leo tunawapa taarifa kwamba tunawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, Bwana Harbinder Singh Sethi na bwana James Rugemalira. Hawa tunawafikisha mahakamani kwa kosa la uhujumu Uchumi na makosa mengine yanayofanana na hayo. Kwa muda mrefu sana nmekuwa naulizwa, Kesi za Escrow zimeishia wapi, Kesi ya IPTL imeishia wapi. Kama tulivyowahi kusema Mwanzo kwamba Taasisi ya kuzuia na kupambana na ruswa, ina jukumu la kimsingi la kupambana na rushwa na makosa ya ufisadi. Kwahiyo katika muendelezo wa majuku yetu, tulichunguza shauri hili kwa muda mrefu, Sasa imefika muda muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa wakuu hawa wa mashauri hayo ya uhujumu uchumi wa nchi yetu mahakamani. Kwahiyo tayari wameshapelekwa mahakamani, na nitoe wito kwa wananchi kwamba Serikali ina nia ya dhati ya kupambana na vitendo vya uhujumu uchumi wa nchi yetu ili wananchi wapate maisha bora zaidi. Na jukumu hili TAKUKURU itaendelea kulitekeleza kwa nguvu zetu zote, kwa waledi wetu wote na kwa umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha kwamba vitendo vya hujuma dhidi ya uchumi wa nchi yetu vinadhibitiwa ili wananchi wapate Maisha Bora”.
kamc1
Harbinder Singh Sethi na James Rugemalila wakiwa katika mahakama ya Kisutu leo.

0 comments:

Post a Comment