F WAZIRI UMMY MWALIMU AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI TANZANIA | Okandablogs

Monday, June 12, 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI TANZANIAWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akutana na balozi mdogo wa marekani Inmi Patterson (Wa pili kutoka Kushoto) katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam mapema asubuhi. Barozi Inmi Patterson ameahidi kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto kwa kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Bima ya Afya kwa watu wote bila kusahau masuala ya uzazi wa mpango.

Pia Mheshimiwa Ummy Mwalimu hakusita kuonesha jitihada za Serikali katika kuhudumia wananchi wake ikiwemo kuongeza ajira mpya kwa watumishi wa Afya ili kuimarisha shughuli za utoaji huduma, Kuendelea kuboresha Miundombinu hususani katika vituo vya Afya ili kuboresha utoaji wa huduma za Upasuaji na Dharura ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. Pia kikao hicho kilihudhuriwa na Brian Rettman kutoka PEPFAR (Wapili Kulia kutoka kwa Waziri), Sharon Cromer kutoka USAID Mission (Wa pili kushoto kutoka kwa Mh. Waziri) na Maestro Evans Mkurugenzi mkazi wa CDC (Wa kwanza Kushoto Kutoka kwa Mh. Waziri).

0 comments:

Post a Comment