WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA IDD EL FITRI KATIKA MSIKITI WA RIADHA MJINI MOSHI.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwasili katika msikiti wa Riadha mjini Moshi kwa ajili ya Swala ya Eid el Fitri iliyofanyik...



Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwasili katika msikiti wa Riadha mjini Moshi kwa ajili ya Swala ya Eid el Fitri iliyofanyika kitaifa mjini Moshi.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi.









Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akishiriki Swala ya Idd el Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki Swala Idd.
Swala ya Idd ikifanyika katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakary Zubery, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Said Mwema (kushoto).

Mshindi wa kuhifadhi Quran tukufu, Ibrahim Mitigo akionesha namna ambavyo alivyohifadhi Quran wakati wa Swala ya Idd el Fitry iliyofanyika katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki Swala ya Idd mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,akizungumza wakati wa Swala ya Idd el Fitry iliyofanyika kitaifa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Mufti wa Tanzania na Sheakh Mkuu, Abubakary Bin Zubery akitoa nasaha zake wakati wa Swala ya Idd iliyofanyika kitaifa mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki katika Swala ya Idd El Fitry iliyofanyika msikiti wa Riadha mjini Moshi

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini)

SERIKALI imeahidi kuongeza kasi katika zoezi la ukamataji wa wahusika wa matukio ya mauaji yaliyotokea Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na kuhakiksha wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana katika baraza la Idd lililofanyika kitaifa katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro ikitanguliwa na Swala ya Idd El Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha.
“Kinachofanyika sasa nikuhakikisha kwanza tunawapata waharifu halisi ilikuepuka kuingiza watu wasio husika, kama vile hao wenye hisia kwamba mauaji haya yanafanywa labda na waislamu hapana.”alisema Mhe. Majaliwa.
Alisema kazi kubwa inayofanywa sasa ni kuchuja na kujua nani hasa anshiriki katika mauaji hayo huku akiwashukuru watanzania ambao tayari wameanza kutoa ushirikiano kwa
kuanza kueleza nani wanahusika katika tukio hilo.
“Kazi yetu ni kuwapeleleza pale ambapo tuna uthibitisho wa ushiriki wao na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kazi hiyo inaendelea vizuri.”alisema Majaliwa.
Mapema katika taarifa ya Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyosomwa na kaimu
katibu Mkuu,Sheakh Salim Amir Abeid alisema Bakwata imeshtushwa na matukio ya mauaji ya kutisha ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani.
Alisema kutokana na matukio hayo Baraza kuu linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo aliyoyataja kutokuwa na hata chembe ya kibinadamu.
“Kumekuwepo na matukio ya kutisha ya mauaji ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani, matukio ambayo yametushtua sana na kuisikitisha mioyo yetu,baraza kuu la waislamu la Tanzania kwanza kabisa linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo ya kinyama yasio na chembe ya kibinadamu hata
kidogo.”alisema Abeid
Alisema Bakwata inasikitishwa na vitendo vyenye viashiria vya kutaka kuichafua dhima nzuri ya Tanzania kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu hasa pale matukio hayo
yanapo husishwa na na Dini ya Kiislamu.
“Uislamu ni dini ya amani upendo kuvumilia na nakuishi pamoja na watu wa imani tofauti na kwamba yeyote afanyae matendo yoyote na kinyama kama hayo katu haiwakilishi uislamu na baraza linawataka waislamu kushikamana.”alisema Abeid.




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA IDD EL FITRI KATIKA MSIKITI WA RIADHA MJINI MOSHI.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA IDD EL FITRI KATIKA MSIKITI WA RIADHA MJINI MOSHI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4qZ4jpXAygIr1-cfrNzm8Hlhde8G69GJysqCbJ5b2d_lHcjSax9yBDEMtOp0ItcX3i6nWsaJRoK7vp6tX2PNUtOPCWK7cRcOilrqaYxgeChkquoSM7S5oGfi6VPRiNN8V1j8VS08h5_Ia/s640/_86A7393.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4qZ4jpXAygIr1-cfrNzm8Hlhde8G69GJysqCbJ5b2d_lHcjSax9yBDEMtOp0ItcX3i6nWsaJRoK7vp6tX2PNUtOPCWK7cRcOilrqaYxgeChkquoSM7S5oGfi6VPRiNN8V1j8VS08h5_Ia/s72-c/_86A7393.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-ashiriki.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-ashiriki.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy