WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA HUDUMA MPYA YA KUPANDIKIZA VIFAA VYA USIKIVU MUHIMBILI

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya muhimbili (MNH), Profesa Lawrence akiongea wakati wa uzi...


unnamed
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya muhimbili (MNH), Profesa Lawrence akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam leo Juni 7, 2017. Pamoja naye ni Museru Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mwenyekiti wa Bodi wa hospitali hiyo, Profesa Charles Majing. 
1
Baadhi ya watalaamu wa upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watu wenye matatizo ya kutosikia wakifuatilia mkutano huo leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utumishi wa Muhimbili, Makwaia Makani akiwa kwenye mkutano huo.
2
Daktari Bingwa wa Masikio, Koo na Pua, Edwin Liyombo wa Muhimbili akieleza jinsi mtu mwenye tatizo la kutosikia anavyofanyiwa upasuaji na kuwekea kifaa cha isikivu.
3
Wataalamu walioshirikiana na madaktari na wauguzi wa Muhimbili kufanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wakiwa kwenye mkutano huo Leo. Kutoka kulia ni Dk Sunil Dutt kutoka India, Dk Hassan Wahba wa chuo Kikuu cha Ain Shams mjini Cairo, Misri, Mohamed El Disouky anayesimamia vifaa vya usikivu Afrika na Mona Amin kutoka Kampuni ya Med-El. Wengine ni wataalamu kutoka Tanzania, Uganda na Kenya.
4
 Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa upandikizaji wa kifaa cha usikivu akimweleza Waziri jinsi  mtoto wake anavyozungumza vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa cha usikivu.

5
 Mama Teodora Myalla akizungumza na mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu baada ya mtoto wake, Mekzedeck Kibona kufanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa cha usikivu juzi katika Hospitali ya Muhimbili. Mtoto huyo sasa anaendelea vizuri.
……………………………………….

 
     Apiga Marufuku Wagonjwa Kutibiwa Nje ya Nchi
 

 

Dar es Salaam, Tanzania. Serikali imesema kwamba kuanzia sasa haitapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa kuwa huduma hiyo imeanza kutolewa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Kauli hiyo imetolewa Leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu katika hospitali hiyo wakati akizindua huduma ya upasuaji wa kupandikiza vivaa vya usikivu (Cochlea Implant).

Ummy alisema kuwa huduma hizo zitakuwa zikitolewa Muhimbili kwa sababu ina madaktari bingwa wenye uwezo wa kufanya upasuaji huo na vifaa vya kisasa na kuokoa gharama kubwa ambazo zilikuwa zikitumika awali kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

Waziri huyo amesema katika hospitali za umma, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu na ya pili kutoa huduma hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.

“Nafarijika Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hii kupitia hospitali ya umma ambayo ni Muhimbili yenye hadhi ya ubingwa wa hali ya juu. Wenzetu Kenya huduma hii inatolewa kwenye hospitali binafsi na inakadiriwa kugharimu dola 31,000 za Marekani ambazi ni sawa na Sh69 milioni za Kitanzania. Hivyo basi tuna kila sababu ya kujipongeza kwa hatua tuliyofikia,”

Akizungumzia gharama, Waziri amesema kuwa mgonjwa mmoja itamgharimu Sh36.9 milioni kwa ajili ya upandikizaji wa kifaa cha usikivu na kwamba kutolewa kwa huduma hiyo katika Hospitali ya Muhimbili itasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa zaidi ya asilimia 60.

Amesema fedha za matibabu zitakazokuwa zikilipwa Muhimbili zitakuwa zikitumika kulipia matibabu kwa wagonjwa wasiokuwa na uwezo. “Ikumbukwe kwamba serikali ilikuwa ikigharamia Sh80 milioni hadi 100 kwa ajili kupandikiza kifaa cha usikivu kwa mtoto mmoja aliyekuwa akipelekwa kutibiwa nje ya nchi,”amesema.

Ummy amesema kuwapo kwa huduma hizo nchini kutawawezesha Watanzania wengi kutibiwa na kuipunguzia serikali gharama ya kupeleka wagonjwa nje kutibiwa na kwamba gharama zitapungua kwa zaidi ya asilimia 60.

Waziri huyo amesema kuwa wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kifedha watapatiwa huduma hiyo kupitia sera ya msamaha kwa watu wasiokuwa na uwezo. “Hospitali ya Muhimbili ina utaratibu mzuri wa kutoa huduma kwa wagonjwa wote wasiokuwa na uwezowa kulipia. Ni vyema wananchi wakatumia utaratibu  huo badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari kulalamika,” amesema waziri huyo.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku mbili mfulilizo kuanzia tarehe 5 hadi 6 Juni, 2017 kwa kushirikiana na wataalamu kutoka India na Misri wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa watoto watano ambao walizaliwa wakiwa na matatizo ya kutosikia.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema kuwa tatizo la usikivu limekuwa likiongezeka katika jamii na kwamba endapo watoto watabainika kuwa na tatizo hilo mapema na kuwekewa vifaa  vya usikivu (Cochlear Implant) wataishi kama watu wengine ambao hawana matatizo na kwamba wasipowekewa vifaa hivyo watakuwa viziwi. “ Ufafiti wa Hospitali ya Muhimbili unaonyesha kuwa kwa mwaka karibu watoto 300 hadi 400 wanahitaji huduma hii hapa nchini. Tunaamini kuwa kuanzishwa kwa huduma hii nchini itawanufaisha wengi,” amesema Profesa Museru.

Profesa Museru ameomba Muhimbili iungwe mkono katika juhudi zake za kuboresha huduma na kwamba iwapo mpango wa kupata madaktari na wauguzi kutoka Cuba utakapokamilika utasaidia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje.

“Tunaomba Serikali itufikirie sisi Muhimbili katika kuwezesha huduma hizi kuwa endelevu kwa kutenga kiasi cha fedha za kutosha ili kuwalipia Watanzania ambao wanahitaji huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu,” amesema Profesa Museru Leo.

Pia, Profesa Museru amefafanua kuwa gharama zilizotumika kwa ajili ya kukarabati, ununuzi wa vifaa tiba, kusomesha wataalamu nje ya nchi, kupanua miundombinu ya utoaji huduma zimegharimu jumla ya Sh13.664 bilioni na kwamba Sh8.855 bilioni zilitumika kununua vifaa vya tiba, Sh 3.858 kwa ajili ya ukarabati na Sh850 milioni kwa ajili ya kusomesha wataalamu.

(PICHA NA JOHN STEPHEN, MNH)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA HUDUMA MPYA YA KUPANDIKIZA VIFAA VYA USIKIVU MUHIMBILI
WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA HUDUMA MPYA YA KUPANDIKIZA VIFAA VYA USIKIVU MUHIMBILI
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/06/unnamed-74.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/waziri-azindua-huduma-mpya-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/waziri-azindua-huduma-mpya-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy