WANANCHI WA CHILONWA, DODOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA DARAJA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na wananchi wa kata ya Chilonwa, wilayani Ch...

chil3
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na wananchi wa kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo mara baada ya kukagua daraja la Chilonwa lililopo mkoani humo.
chil1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, akisalimia wananchi wa kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma alipotembelea wilayani hapo leo, ikiwa ni kutekeleza ahadi yake ya kukagua daraja la Chilonwa kwa Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga.  
 
chil2
Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (kushoto kwa Mbunge), alipofika jimboni hapo kukagua daraja la Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo.
chil4
Muonekano wa Daraja la Chilonwa lililopo kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Daraja hilo ni kiungo kati ya mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
chil5
Sehemu ya daraja la Chilonwa iliyoathirika kutokana na shughuli za kibinaadamu kama vile kilimo na  hivyo kupelekea kwa daraja hilo kufukiwa na mchanga na kuwa fupi.
………………………………………………………………..
Wananchi wa kata ya Chilonwa, wilaya Chamwino mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kujenga daraja la Chilonwa lililopo katika kata hiyo ili kutatua kero ya usafiri  kwa wananchi  hao na maeneo jirani hususan katika kipindi cha masika.
Wakieleza kero yao kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wananchi hao wamesema wanaamini kuwa ujio wa Naibu Waziri huyo katika kata yao kutaleta ufumbuzi  wa kero hiyo.
“Tunaamini sasa tutapata mwarobaini wa daraja hili kwani tatizo hili ni la muda mrefu, siku hadi siku daraja linakuwa fupi kutokana na kufukiwa na mchanga na hivyo hupelekea maji kujaa darajani hapa kipindi cha masika na watu kushindwa kuvuka”, amesema mmoja wa wananchi hao.
Aidha, wananchi hao wamemwomba Naibu Waziri huyo kurekebisha daraja hilo kwa kulijenga juu zaidi ili kupitisha maji na kupitika katika vipindi vyote vya mwaka kutokana na kwamba lililopo sasa lipo chini zaidi mara baada ya kufukiwa na mchanga.
Wananchi hao wameeleza masikitiko yao kwa Naibu Waziri huyo hususan katika kipindi cha masika ambapo wamesema hutumia kiasi cha shilingi elfu kumi kuvushwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wengine hupoteza maisha wakiwa wanavuka.
Sambamba na hilo wananchi hao wamependekeza kuwa ujenzi wa daraja hilo uhusishe wataalamu waliobobea na ambao watahakikisha daraja hilo linakamilika mapema na kwa viwango.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ngonyani, amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kufanya shughuli za kibinaadamu kama kilimo katika njia ya mto kwani hali hiyo hupelekea udongo kumung’unyuka na hatimaye mchanga kufunika daraja.
Amemtaka Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, kwa kushirikiana na viongozi wa kata na kijiji kuhamasisha wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinaadamu kando ya mto.
Amefafanua kuwa Wizara yake kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani  Dodoma itahakikisha kwanza ina utengeneza mto huo kwa kuelekeza maji yote katika mto.
Naye, Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kutembelea jimboni hapo na kuahidi kuwasimamia wananchi wake katika kulinda miundombinu hiyo.  
Naibu Waziri Ngonyani leo ametembelea na kukagua Daraja la Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni kutekeleza ahadi yake ya kutembelea na kukagua daraja hilo kwa Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga. 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANANCHI WA CHILONWA, DODOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA DARAJA
WANANCHI WA CHILONWA, DODOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA DARAJA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/06/chil3.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/wananchi-wa-chilonwa-dodoma-waiomba.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/wananchi-wa-chilonwa-dodoma-waiomba.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy