VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA BINAFSI WAMETAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA – PROF MOHAMED JANABI

Na Mwandishi wetu – JKCI Viongozi wa mashirika ya Umma na Binafsi  wametakiwa kujenga mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara i...


Na Mwandishi wetu – JKCI
Viongozi wa mashirika ya Umma na Binafsi  wametakiwa kujenga mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara ili kufahamu  kama wana magonjwa yanayowasumbua au la na kwa kufanya hivyo wataweza  kupata matibabu kwa wakati.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya upimaji wa Afya zao.
 Prof. Janabi alisema baadhi ya viongozi  hawana mazoea ya kupima afya zao japo mara moja kwa mwaka na inapotokea wamegundulika  kuwa na tatizo  la ugonjwa huwa ni  kubwa na limeshaleta madhara mwilini,   na wakati  mwingine huwa  ni vigumu kutibika lakini  tatizo kama hilo likigundulika  mapema katika hatua ya awali  huwa ni  rahisi kutibika.
 Akizungumzia kuhusu magonjwa ya Moyo Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema ni muhimu mgonjwa afuate maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa aliyopewa na daktari wake kwani kuna baadhi ya wagonjwa wamekuwa na tabia ya kuacha kutumia dawa pindi wanapojiona wamepata naafuu jambo ambalo siyo sahihi.
 Akielezea  jinsi ya kujikinga na magonjwa ya Moyo kwa upande wa chakula Afisa Lishe kutoka JKCI Louisa Shem  alisema ni muhimu kupunguza utumiaji wa vyakula vya mafuta kupita kiasi hasa mafuta yatokananyo na wanyama, kutumia vyakula vya nafaka zisizokobolewa.
 Kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji wa bidhaa zitokanazo na tumbaku ikiwemo sigara, kufanya mazoezi ya mwili angalau nusu saa kwa siku na kupunguza matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama Kazini kutoka  NHC Dkt. Yothan Mackenzie  alisema hivi karibuni walikuwa na mkutano wa Baraza la Wafanyakazi katika mkutano huo kulikuwa na mada ya ulaji na afya wakaona ni vyema mada hiyo iende sambamba na upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Moyo.
 Dkt. Mackenzie alisema wanawapima viongozi hao kwa awamu hadi sasa jumla ya wakurugenzi na wakuu wa vitengo 14 wamepima na kujuwa afya zao na viongozi wengine wataendelea kupima kwani Shirika lao linaamini kuwa  mfanyakazi akiwa na afya njema ataweza kufanya kazi zake vizuri.
 Baadhi ya magonjwa waliyopima viongozi hao ni pamoja na  Moyo, tezi dume, figo na sukari.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA BINAFSI WAMETAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA – PROF MOHAMED JANABI
VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA BINAFSI WAMETAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA – PROF MOHAMED JANABI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTaTJT-sGop4WIE5o2pPtFrSqM-51K6IH1jG-Wuh1IPsyhHbLuXoWlsotAw3bqaDEc4gy-6v3lLZQ3oilyD-HwPSA93Ncq5vPNLqmP0m96_znI1ETH5n3GEmEJTvlBG6d2eaPEW5RBmwk/s320/0002.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTaTJT-sGop4WIE5o2pPtFrSqM-51K6IH1jG-Wuh1IPsyhHbLuXoWlsotAw3bqaDEc4gy-6v3lLZQ3oilyD-HwPSA93Ncq5vPNLqmP0m96_znI1ETH5n3GEmEJTvlBG6d2eaPEW5RBmwk/s72-c/0002.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/viongozi-wa-mashirika-ya-umma-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/viongozi-wa-mashirika-ya-umma-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy