F VIDEO MOAHEMMED DEWJI AMREJESHA EMMANUEL OKWI SOMBA SC | RobertOkanda

Monday, June 26, 2017

VIDEO MOAHEMMED DEWJI AMREJESHA EMMANUEL OKWI SOMBA SC

Mwanachama wa Simba Sports Club na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji MO ametoa zawadi ya sikukuu ya Eid kwa mashabiki wa Simba SC kwa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi.

Katika taarifa ambayo MO Dewji ameitoa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, MO Dewji amesema usajili wa Okwi ambaye amewahi kuichezea Simba SC kwa nyakati mbili tofauti ni zawadi kwa ajili ya mashabiki wa Simba katika sikukuu ya Eid ambayo itasherehekewa jumatatu ya Juni, 26.

"Naomba nitoe zawadi kwa ajili ya mashabiki wa Simba SC kwa kuwapa ndugu yetu Okwi," alisema MO Dewji baada ya kukamilika kwa usajili wa Okwi.

Kwa upande wa Okwi alisema amefurahi kurejea Simba na kuwaahidi mashabiki kutekeleza wajibu wake ili kuiwezesha timu yake kushinda makombe ya mashindano ambayo itakuwa ikishiriki lakini pia akimshukuru MO Dewji kwa kufanikisha uhamisho wake.

“Nimekuja kupambana na kuhakikisha tunachukua ubingwa ... namshukuru sana bosi MO Dewji kwa kufanikisha huu uhamisho wa kuja Simba," alisema Okwi.
VIDEO: Mohammed Dewji amrejesha Emmanuel Okwi Simba SC - (CODES)

0 comments:

Post a Comment