TIC YAWAFUNDA WAJASIRIAMALI

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uwekezaji Bw. John Mnali akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunz...

TIC1
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uwekezaji Bw. John Mnali akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam.
 
TIC2
Baadhi ya wajasirimali wakifuatilia mafunzo hayo  yaliyoandaliwa na Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC).
TIC3
Mmoja wa wajasiriamali hao Bibi  Neli William akishukuru TIC kwa kuandaa mafunzo hayo.
(Picha na Frank Shija)
………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewataka Wajasiriamali nchini kujiamini na kutumia fursa zilizopo ili kukuza biashara zao na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uwekezaji wa TIC, Bw. John Mnali AMETOA WITO HUO wakAti wa mafunzo ya siku moja kwa wajasiriamali yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kuzingatia ubora.
Akifafanua Mnali amesema mafunzo hayo ni fursa kwa wajasiriamali wakati na wadogo kukutana na wajasiriamali wakubwa waliowekeza hapa nchini hali itakayochochea kuongeza ubora wa bidhaa na huduma wanazotoa.
“Jukumu la Kituo cha Uwekezaji hapa nchini ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali wadogo na wakati wanazalisha bidhaa zitakazotumiwa na makampuni makubwa ya wawekezaji”, alisisitiza Mnali
Katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanakuza mitaji yao Kituo cha Uwekezaji kimeshirikisha taasisi za fedha katika mafunzo hayo ili kuwapa fursa wajasiriamali wadogo na wakati kupata mikopo itakayo wawezesha kukuza uzalishaji wao.
Kwa upande wake mmoja wa wajasiriamali hao, Bi.  Neli William amesema kuwa wajasiriamali Watanzania wamekuwa waoga kudhubutu kuzalisha bidhaa kwa wingi na kuzitangaza ili kukuza soko la bidhaa hizo.
“Nakishukuru Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa mafunzo haya kwa kuwa yametujengea uwezo ambao utasaidia kukuza uzalishaji wetu na kuongeza tija”, alieleza Bi.  Neli.
Aliongeza kuwa kila siku anao uwezo wa kuzalisha trei 70 za mayai hivyo baada ya mafunzo dhamira yake ni kuongeza kiwango cha uzalishaji.
 Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimekuwa kikitoa mafunzo kwa wajasiriamali hapa nchini ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji ya soko.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIC YAWAFUNDA WAJASIRIAMALI
TIC YAWAFUNDA WAJASIRIAMALI
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/06/TIC1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/tic-yawafunda-wajasiriamali.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/tic-yawafunda-wajasiriamali.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy