TAIFA LA WATU WAADILIFU HUANZIA KWENYE FAMILIA – WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kushoto) akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu  Mizengo Pinda na Mkewe Tunu Pinda walipo mpokea ...


pind1Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kushoto) akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu  Mizengo Pinda na Mkewe Tunu Pinda walipo mpokea  katika makazi yao yaliyopo Zuzu Nnje Kidogo ya  Mjini Dodoma June 17, 2017 kuhudhuria Misa ya kumbukumbu ya Marehemu Mzee Exavery Pinda Baba Mzazi wa Mizengo  Pinda, Pamoja na kuongoza  Uchangiaji wa Ujenzi wa Nyumba ya Paroko na Ukarabati wa Kanisa la Parokia ya ZUZU. (Picha na Ofisi  ya  Waziri Mkuu)
pind2Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa  kwaniaba  ya familia yake  akimkabidhi Mchango wa Shilingi Milioni Kumi Waziri Mkuu  Mstaafu  Mizengo  Pinda. Kwa ajili ya kuchangia ujenzi  wa  Nyumba  ya Paroko  pamoja nakufanyia Ukarabati  wa  Kanisa  Parokia ya ZUZU Dodoma, Kushoto  ni  Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco  Msaga. Harambe hiyo  imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu  Pinda  yaliyopo ZUZU Nje kidogo ya Mjini Dodoma
pind3Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiwaonyesha Wageni waalikwa Shilingi Milioni Kumi Mchango alizo kabidhiwa na Wziri Mkuu  Kassimu Majaliwa kwa niaba ya Familia yake, Kwa ajili ya kuchangia ujenzi  wa  Nyumba ya Paroko pamoja nakufanyia Ukarabati  wa  Kanisa  Parokia ya Zinje (ZUZU) Dodoma, Kushoto  ni  Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma  Baba  Chesco  Msaga. Harambe hiyo  imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu  Pinda  yaliyopo  ZUZU Nnje kidogo ya mjini Dodoma
………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wazazi wana jukumu la kulea watoto kwenye misingi ya kumcha Mungu ili Taifa liweze kuwa na watu waadilifu na wachapakazi. 
“Taifa la watu waadilifu na wachapakazi huanzia katika ngazi ya familia. Kama kaya zetu haziishi kwa uadilifu, ni vigumu sana kuwa na Taifa lenye wananchi waadilifu. Ni muhimu basi familia zetu zihakikishe kuwa tunakuwa na watoto wenye hofu ya Mungu na wenye kumcha Mungu,” alisema.
Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Juni 17, 2017) wakati akizungumza na wageni waliohudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa na nyumba ya Paroko katika Parokia Teule ya Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma. 
Harambee hiyo ilitanguliwa na ibada ya misa ya shukrani kwa ajili ya marehemu Mzee Xavery Mizengo Pinda, ambaye ni baba yake, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Peter Pinda. Mzee Xavery Pinda alifariki Novemba 27, mwaka jana katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na kuzikwa kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele, Katavi.
Waziri Mkuu alisema wazazi wanapaswa kujitathmini juu ya malezi ya watoto wao na kujihoji kama wamepata malezi yanayostahili. “Kupitia funzo tulilolipata leo, tujitathmini kuhusu makuzi ya watoto wetu. Je watoto wetu wanapata malezi stahiki? Je tunawalea katika misingi ya kutoa kwa ajili ya Mungu au tunawafundisha wajilimbikizie mali? Je, tunawahoji watoto wetu kuhusu utajiri wanaoupata ghafla? Au tunawapongeza na kufurahia bila kujua wanapata wapi utajiri huo?,” alihoji.
“Nitumie nafasi hii kuwasihi wazazi wote kwamba tujitahidi kuwekeza katika malezi ya watoto wetu. Ili tuwe kioo cha aina ya Taifa tunalotaka kulijenga, hatuna budi kuwalea watoto wetu katika misingi ya imani, uadilifu na uzalendo mkubwa kwa nchi yetu,” alisisitiza.
Katika harambee hiyo, Waziri Mkuu na mke wake walichangia sh. milioni 10 ambapo jumla ya sh. milioni 160 zilikusanywa. Kati ya hizo, sh. 111,150,000 zilikuwa ni ahadi, sh. 38,447,000 zilikuwa ni fedha taslimu na sh. 10,403,000 zilikuwa ni vifaa vya ujenzi.
Mapema, akiongoza ibada ya shukrani, Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Padre Chesco Msaga alisema kila mtu anapaswa kumshukuru Mungu kwani hakuna mwanadamu anayeweza kudai kuwa yuko jinsi alivyo kwa sababu ya akili zake.  
“Hata sisi tunasahau kumshukuru Mungu hasa pale mambo yetu yanapotunyookea. Tunadhani ni kwa akili zetu ndiyo mambo yetu yananyooka. Tunapaswa tukumbuke kuwa maishayetu yapo mikononi mwa Mungu, na yeye ndiye anajua njia zetu,” alisema akirejea mfano wa wakoma 10 walioponywa na Bwana Yesu na mmoja tu ndiye alirudi kushukuru.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda alisema harambee hiyo inafuatia uamuzi wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya wa kuiteua Zuzu iwe parokia. 
“Sasa hivi tulikuwa na Kigango. Kuteuliwa kuwa parokia maana yake tutakuwa na padre anakaa hapa Zuzu saa 24 na tutakuwa na ibada kila Jumapili, na katikati ya wiki kadri ratiba zitakavyoruhusu. 
“Kikubwa tunachopaswa kufanya kufuatia uamuzi huo, ni kuhakikisha kuwa mapadre wana nyumba ya kuishi. Sasa hivi, wa kwetu anakaa Dodoma mjini. Kwa hiyo tuna kazi ya kukarabati kanisa, lakini kwanza tukamilishe ujenzi wa nyumba ya mapadri,” alisema wakati akielezea madhumuni ya harambee hiyo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAIFA LA WATU WAADILIFU HUANZIA KWENYE FAMILIA – WAZIRI MKUU
TAIFA LA WATU WAADILIFU HUANZIA KWENYE FAMILIA – WAZIRI MKUU
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/06/pind1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/taifa-la-watu-waadilifu-huanzia-kwenye.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/taifa-la-watu-waadilifu-huanzia-kwenye.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy