F SHEREHE ZA UFUNGAJI WA MASHINDANO YA KOMBE LA MKUU WA MAJESHI (CDF CUP) | Okandablogs

Friday, June 2, 2017

SHEREHE ZA UFUNGAJI WA MASHINDANO YA KOMBE LA MKUU WA MAJESHI (CDF CUP)

logo[3]
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463    Sanduku la Posta 9203,
Telex                  : 41051            DAR ES SALAAM, 02 June 2017
Tele Fax        : 2153426
Barua pepe    : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Tovuti        : www.tpdf.mil.tz
Wito wa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa wito kwa vyombo vya Habari ili kufanya coverage ya kufungwaji wa mashindano ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP) ambayo yanatarajiwa kufungwa  rasmi tarehe 04 Juni 2017 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.  Mgeni rasmi  anatarajiwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, kuanzia Saa nne (4:00) kamili asubuhi.
Lengo la mashindano hayo lilikuwa kudumisha mshikamano, kuvumbua na kukuza vipaji na kupata timu itakayo wakilisha Jeshi na Taifa kwa ujumla katika mashindano ya michezo ya Majeshi na Utamaduni kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka huu mashindano yanayotarajiwa kufanyika nchini Burundi mwezi wa nane 2017.Ukiwa mdau wa habari inaombwa chombo chako kufanya ‘coverage’ katika tukio hili muhimu.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.


0 comments:

Post a Comment