SBL YAZINDUA MRADI WA MAJI KWA WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia), akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni H...




Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia), akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni Hamisi Ramadhani wakati wa uzinduzi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68  uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Miradi Endelevu wa SBL, Hawa Ladha. 



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) na Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo.



Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako , akisoma hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo. Kulia ni Diwani wa Viti Maalumu, Mwanakombo Mwinyimvua na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa katika eneo hilo.

Hii ni Crew nzima ya Kampuni ya Concept waratibu wa masuala yote ya mawasiliano ya SBL.
Mwonekano wa mradi huo.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyanja akizungumza kwenye hafla hiyo kuhusu mradi huo.

Uzinduzi ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

 KAMPUNI ya Bia Serengeti leo
imezindua  mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68  uliopo
katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam  ikiwa
ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.

Ukiwa na uwezo kwa  kuhudumia
watu 4,000 mradi huo unajumuisha  kisima  pamoja na mifumo
yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la
maji  ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila masaa ishirini
na nne.

Akizungumza katika  hafla ya
uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie  alisema kuwa
mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni miongoni
mwa  mikakati kama hiyo  ambayo kampuni ya
bia  imeiendesha  katika mikoa ya  Iringa,
Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha  zaidi
ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.

 Weesie alisema kwamba mradi wa
Chang’ombe  sio tu kwamba  utaboresha afya za wakazi wa
eneo hilo bali pia  utaongeza tija kiuchumi, “hususani kwa watoto wa
kike na wanawake  ambao  hawatahitaji kutumia saa
nyingi  kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya
kuhudhuria shule wakiwa huru.”

 “SBL  ina sera iliyojikita
katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne
ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo
lake  kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Weesie akielezea
vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na
Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

Mkurugenzi huyo Mtedaji aliendelea
kusema SBL ina programu ya kilimo  ambayo katika kipindi cha miaka
mitatu iliyopita  imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa
kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na
maisha ya jumuia zao.

Weesie  alisema kutokana na
juhudi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa
wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 10,000 na hili
limechangia  katika kukua kwa kampuni  na
kukuza  kipato cha wakulima.”



Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia
katika kukua kwa uchumi wa taifa  kupitia  malipo ya kodi
ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa
hususani  katika kutoa  huduma  ya
maji  safi na salama ndani ya nchi.”



(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SBL YAZINDUA MRADI WA MAJI KWA WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM
SBL YAZINDUA MRADI WA MAJI KWA WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiOihnuELPfcQg7iP7v7uVC7AHzqKabU8oIjWjhfO646qnDyboNVeDkr2gCDUOriP62X9LH5_8ne5fcEmWeYjI-atPd4uAUSWeWMdfPzfqM3W110ZrD2FiDBUuKUezQqAMaDNc664O9u8oq/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiOihnuELPfcQg7iP7v7uVC7AHzqKabU8oIjWjhfO646qnDyboNVeDkr2gCDUOriP62X9LH5_8ne5fcEmWeYjI-atPd4uAUSWeWMdfPzfqM3W110ZrD2FiDBUuKUezQqAMaDNc664O9u8oq/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/sbl-yazindua-mradi-wa-maji-kwa-wakazi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/sbl-yazindua-mradi-wa-maji-kwa-wakazi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy