RAIS MAGUFULI AIPONGEZA PSPF KWA KUBUNI MAFUNZO YA KUWATAYARISHA WASTAAFU WATARAJIWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sukuhu Hassan, (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pens...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sukuhu Hassan, (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, huku Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, mara baada ya kufungua rasmi semina ya siku mbili kwa wastaafu watarajiwa kutoka wilaya zote saba za mkoa wa Mwana leo Juni 3, 2017. Semina hiyo inayolenga kuwanadaa wastaafu watarajiwa, imetayarishwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF. 

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa hatua yake ya kuwataayarisha watumishi wa Umma wanaokaribia kustaafu kwa kuwapatia semina ya mafunzo ili wastaafu kwa amani.
Akifungua rasmi semina ya siku mbili kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na PSPF kwenye ukumnbi wa chuo cha Watumishi wa BoT jijini Mwanza leo Juni 3, 2017, Makamu wa rais Mama Samia Suuhu Hassan, (pichani juu), alisema,  “Rais amependezwa sana na jitihada zenu za leo za kuhakikisha mnawatayarisha wastaafu wetu watarajiwa, na amesema nay eye asingekuwa rais basi hapana shaka kuwa nae leo angekuwa miongoni mwa wanufaika wa semina hii, hongereni sana kwa kubuni wazo hili.” Alisema mama Samia.
Kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi” na kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, kwa mwaka wa 2017/018 Mfuko unatarajia kulipa Wastaafu 9,552  Mafao yanayofikia Shilingi Trilioni 1.3.
Aidha Rais Magufuli amesema katika salamu zake zilizosomwa na Makamu wa Rais kwa washiriki wa semina hiyo kuwa, anaipongeza PSPF kwa kuendelea kumuunga mkono katika jitihada zake za kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025 na kuwa asilimia 40 ya ajira itatoka kwenye viwanda hivi.
Katika semina hiyo, pamoja na mambo mengine,washiriki wamepatiwa mafunzo ya uanzishaji viwanda vidogo vidogo toka kwa maafisa wa Shirika la Viwanda Vidogo vidogo nchini SIDO.
Aidha  Makamu wa Rais kwa upande wake alisema, amefurahishwa na ubunifu huo na kuitaka mifuko mingine kuiga mfano huo kwani una manufaa makubwa katika kuwandaa watumishi wa umma wanapojiandaa kustaafu ili kuondoa hofu ya namna ya kuishi baada ya utumishi wa umma.
“Lakini niungane na Naibu waziri wa Fedha na Mipango, aliysema ninyi sio wastaafu watarajiwa bali ni wawekezaji watarajiwa, na hivyo nawaasa, fedha mtakazopata mzitumie kwa malengo yatakayoboresha maisha yenu, lakini pia akina baba nao watumie fedha hizo kuanzisha miradi mipya na sio kuongeza wake.” Alsiema Makamu wa Rais.
Akieleza zaidi, Makamu wa Rais amewataka washiriki hao kubadili mfumo wa matumizi ya fedha ili kueldana na hali halisi, ikiwa ni pamoja na kutotumia fedha ovyo kwa matumizi makubwa yasiyo na manufaa.

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amewatia shime wastaafu hao watarajiwa kuwa wachangamkie fursa mbalimbali zinazojitokeza kutokana na semina hii ambapo wadau wa PSPF, kama vile taasisi za kifedha zimetoa elimu ya huduma wazitoazo ambazo pia zinaweza kuwa na manufaa kwao.
Lakini ninyi sio wastaafu watarajiwa ninyi ni wastaafu wawekezaji hivyo mmestaafu utumishi wa umma na hamjastaafu kazi.” Alsiema Dkt. Kijaji.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (pichani juu), akitoa taarifa yake alisema, “Nchi yetu ina jumla ya Mifuko ya Pensheni mitano kwa Tanzania bara na mmoja kwa Tanzania Visiwani, pamoja na idadi hii ya Mifuko, PSPF ndio Mfuko wenye idadi kubwa ya wastaafu kwa mwaka na pia daftari kubwa la malipo ya pensheni kila mwezi.” Alifafanua na kuongeza
“PSPF inahudumia wanachama 403,605 na wastaafu wategemezi 62,892 ambao kwa kiasi nkikubwa ni watumishi wa umma wakiwemo walimu, askari polisi, askari magereza, aidha kwa upande wa uchangiaji wa Hiari Mfuko una wanachama 86,900 na hii ni kuhakikisha Mfuko unatekeleza kwa vitendo juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wengi zaidi wanafaidika na mfumo wa hifadhi ya jamii nchini.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, akitoa shukrani za Mfuko. "Ni wazi kuwa matokeo ya mafanikio yanayopelekea PSPF kuvutia makundi mbalimbali ya jamii yetu yasingepatikana bila ya ushirikiano mzuri kutoka kwa Wanachama wetu, Waajiri, Taasisi mbalimbali na wadau wengine kwa ujumla.Napenda nikupongeze Mhe. Makamu wa Rais kwa mara pili, umeungana nasi katika tukio hili juhimu la kutoa semina kwa wanachama wetu wanaotarajia kustaafu, hii ni faraja kubwa kwetu." Alisema Bw. Muhoji.


Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, (wakwanza kulia), akionyesha vipeperushi na vijitabu vyenye maelezo ya huduma za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, mara baada ya kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na PSPF na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha watumishi wa BoT, jijini Mwanza leo Juni 3, 2017. Wengine pichani ni Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (wapili kulia), Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza…..na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu.


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akipokea mfuko wenye vipeperushi na machapisho mbalimbali yenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Bw. Adam Mayingu

 Furaha ya hotuba nzuri
  Furaha ya hotuba nzuri
 Kutoka kushoto ni ni Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw. Mohammed Salim, Meneja Mipango na Utafiti, wa PSPF, Bw. Luseshelo  Njeje, na Mkurugenzi wa Masoko Mfuko wa UTT-AMIS, Bw. Daudi Mbaga, wakifurahia jambo
 Mshiriki wa semina akionyesha furaha yake kufuatia hotuba murua ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
 Washiriki wakifuatilia semina
 Huyu ni mmoja wa wastaafu ambaye sasa anafaidika na Mafao ya PSPF, akionyesha shukrani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sukuhu Hassan, akipewa maelezo ya utangulizi kuhusu semina kwa wastaafu watarajiwa toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, ambapo baadaye Mama Samia lifungua rasmi semina hiyo iliyofanyika ukumbi wa chuo cha watumishi wa BoT, jijini Mwanza leo Juni 3, 2017. Zaidi ya wastaafu watarajiwa 450 wanashiriki semina hiyo

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe. John Mongela akiongea
 Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza nao walikuwepo
 Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, amakamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
 Makamu wa Rais, akisindikizwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Kijaji, Mkurugenzi Mkuu Mayingu, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Mongela


Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, (wapili kulia), akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, wakati akiwasili ukumbi wa chuo cha watumishi wa BoT jijini Mwanza leo Juni 3, 2017 kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko huo na kuwaleta pamoja washiriki zaidi ya 450n kutoka wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza. Anayeshuhudia wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu.

 Sehemu ya washiriki wa semina
 Mkurugenzi wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (kushoto) ambaye anasimamia Mipango na Uwekezaji na Bi. Neema Muro anayeshughulikia Uendeshaji wakifuatilia semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa utulivu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na wasemaji wakionhozwa na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AIPONGEZA PSPF KWA KUBUNI MAFUNZO YA KUWATAYARISHA WASTAAFU WATARAJIWA
RAIS MAGUFULI AIPONGEZA PSPF KWA KUBUNI MAFUNZO YA KUWATAYARISHA WASTAAFU WATARAJIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsHGAVvToHF7XM-qMgCpdhe7wV05O1-K-jcENefMSz7B5GYnMFPWeRgsBRytDwCn8HdflOamp939DRPVLTKUJus9Q0E4yhQq8GUJzHr4-WeQIz3SmCXxQiib6ZhfCqC8W-xTXH8DJw5hs/s640/5R5A4559.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsHGAVvToHF7XM-qMgCpdhe7wV05O1-K-jcENefMSz7B5GYnMFPWeRgsBRytDwCn8HdflOamp939DRPVLTKUJus9Q0E4yhQq8GUJzHr4-WeQIz3SmCXxQiib6ZhfCqC8W-xTXH8DJw5hs/s72-c/5R5A4559.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/rais-magufuli-aipongeza-pspf-kwa-kubuni.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/rais-magufuli-aipongeza-pspf-kwa-kubuni.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy