RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA JOPO LA WATAALAMU WA NISHATI NA MIUNDOMBINU YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME NA WATUMISHI WA ILIYOKUWA BRN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la   wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miund...


wami7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la   wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2017.
 
wami1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea  na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN  alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2017.
 
wami2 wami3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na  na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN) alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2017.
 
wami4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na  na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2017.
 
wami5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la   wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2017.
 
wami6
…………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Juni, 2017 ameagana na wafanyakazi wa iliyokuwa Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (President’s Delivery Bureau – PDB) ambao wamehamishiwa katika ofisi na taasisi nyingine za Serikali kwa ajili ya kuendelea na utumishi wa umma.
Wafanyakazi hawa ndio walikuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN).
Mhe. Rais Magufuli amekutana na wafanyakazi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo amewashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya wakiwa PDB na amewataka kuendelea kulitumikia Taifa kwa juhudi na maarifa wakiwa katika ofisi nyingine walizopangiwa.
“Natambua kuwa nyie ni wafanyakazi wazuri wenye ujuzi na maarifa muhimu kwa ajili ya Taifa letu. Mmetoa mchango mkubwa mlipokuwa PDB nategemea mtaendelea hivyo na hata zaidi katika ofisi mbalimbali mlizopangiwa, mkachape kazi kwa kutanguliza maslahi ya Watanzania” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na timu ya wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme.
Mhe. Rais Magufuli amekutana na wataalamu hao ikiwa ni utekelezaji wa nia yake ya kuhakikisha mradi huo unaanza kujengwa haraka iwezekanavyo na kuzalisha umeme mwingi utakaosaidia kuharakisha maendeleo hapa nchini, hususani ujenzi wa viwanda.
“Kesho Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn anawatuma wataalamu wake waliojenga mradi mkubwa wa bwawa la maji la kuzalisha umeme kule Ethiopia, wakiwa hapa mtakutana nao na mtabadilishana uzoefu, nataka na sisi tusichelewe, tuzalishe umeme utusaidie kwenye ujenzi wa viwanda” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Juni, 2017

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA JOPO LA WATAALAMU WA NISHATI NA MIUNDOMBINU YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME NA WATUMISHI WA ILIYOKUWA BRN
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA JOPO LA WATAALAMU WA NISHATI NA MIUNDOMBINU YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME NA WATUMISHI WA ILIYOKUWA BRN
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/06/wami7.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/rais-dkt-magufuli-akutana-na-jopo-la.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/rais-dkt-magufuli-akutana-na-jopo-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy