PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufu...







NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo kwa
watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), jijini Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, kwenye ufunguzi wa semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Gabriel Silayo
alisema, semina hiyo inalenga kuwandaa kwa kuwapa mafunzo watumishi wa umma ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni, ili hatimaye wastaafu kwa amani.
“Na kwa kufanikisha hilo, tunao maafisa wetu watatoa mada mbalimbali, wapo washirika wetu, SIDO, na mabenki kama vile NMB, CRDB, TPB, MCB na UTT, ambao watatoa elimu ya namna bora ya kutunza na kutumia fedha zako za mafao.” Alibainisha Bw. Silayo.
Bw. Silayo pia alisema, kwa kutambua kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi”. “Na ndio maana tumewaleta SIDO hapa ili
wawaelimishe jinsi mtakavyoweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo baada ya kustaafu utumishi wa umma na ndugu zangu napenda niwahakikishie hilo linawezekana.” Alisema
Alisema semina hiyo itakuwa ya siku mbili na kwamba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ataifungua rasmi kesho Jumamosi
Juni 2, 2017.
Zaidi ya watumishi 300 kutoka sekta mbalimbali za utumishi wa umma kwenye wilaya zote za mkoa wa  Mwanza wanahudhuria semina hiyo ya mafunzo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
 Meneja Pensheni wa PSPF, Bw. Mohammed Salim, akitoa mada juu ya maandalizi na fursa za wastaafu.
 Afisa Mwandamizi wa Utafiti wa PSPF, Bw. Mapesi Maagi, akigawa vitendea kazi kwa washiriki wa semina mwanzoni mwa mafunzo hayo


 Bw. Silayo, (Kushoto), akiteta jambo na Meenja wa Mipango na Utafiti wa PSPF, Bw. Luseshele Njeje.
 Mshiriki akizunguzma wakati wa semina hiyo
 Afisa Uhusino Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akitoa utaratibu wa namna semina hiyo itakavyoendeshwa
Mshiriki akinukuu kilichokuwa kikiendelea
 Wanasemina wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa
 Baadhi ya wadau wa PSPF, na washiriki wa semina wakifuatilia mada zilziokuwa zikitolewa
 Washiriki wa semina wakiwa kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo BoT jijini Mwanza
 Bw. Silayo, (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja wa Fedha wa Mfuko huo, Bw.Lihami Masoli
 Kuonyesha semina hiyo ilikuwa muhimu kwa wastaafu hawa watarajiwa, mshiriki wa semina akinakili kwa uangalifu mkubwa yaliyokuwa yakielezwa (mafunzo)
 Afisa Mfawidhi wa PSPF, mkoani Mwanza, Bw.Salim Salum, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo na katikati ni Meenja wa Pensheni wa Mfuko huo, Bw. Mohammed Salim
 Sehemu ya washiriki wa semina
 Mshiriki akipitia ratiba
Washiriki hawa wakipitia vipeperushi vya PSPF vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA
PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjp7homv9bG08FS9-0sPDvEUBct32Dr2zg9FBV_0QEO5CCxBC_AP_hPK9d3G2_EF61kBq_oY0KvLD6sB0jy_IrKvvXRzZov_jG_OVmUqcs8wjA9s3z1MBzO2ySQ3zFMfWIcCgBv-fiUlM0/s640/5R5A3181.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjp7homv9bG08FS9-0sPDvEUBct32Dr2zg9FBV_0QEO5CCxBC_AP_hPK9d3G2_EF61kBq_oY0KvLD6sB0jy_IrKvvXRzZov_jG_OVmUqcs8wjA9s3z1MBzO2ySQ3zFMfWIcCgBv-fiUlM0/s72-c/5R5A3181.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/pspf-yawapiga-msasa-wastaafu-watarajiwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/pspf-yawapiga-msasa-wastaafu-watarajiwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy