F NGULI WA EVERTON LEON OSMAN AZINDUA PROGRAMU YA SOKA LA VIJANA LEO JIJINI DAR | Okandablogs

Thursday, June 1, 2017

NGULI WA EVERTON LEON OSMAN AZINDUA PROGRAMU YA SOKA LA VIJANA LEO JIJINI DAR

Wanamichezo Watakiwa Kuzingatia Nidhamu
Na Lorietha Laurence
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wadau wa michezo nchini kuzingatia nidhamu na uvumilivu ili kufikia malengo ya klabu zao.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harisson Mwakyembe leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia ujio wa klabu ya Everton nchini chini ya uratibu wa Kampuni ya SportPesa.
Katika mkutano huo, Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa ujio wa uongozi wa timu ya Everton ni fursa kubwa kwa vilabu vya mpira wa miguu nchini katika  kujifunza mbinu mbalimbali za  kuendeleza na kukuza vipaji vya wachezaji wake.
“Ujio huu ni muhimu na elimu tosha kwa vilabu vyetu nchini katika kuhakikisha vipaji vya wanamichezo vinakuzwa na kuendelezwa ili kufanikisha maendeleo ya sekta ya michezo “alisema Dkt.Mwakyembe.
Alisema mbali na elimu itakayopatikana kutoka kwa timu na uongozi wa Everton, ni fursa nzuri katika sekta ya Utalii kwa kuwa wageni hao wataweza kutembelea Mbuga za Wanyama,Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine mbalimbali vya kimichezo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Everton, Robert Elstone amesema kuwa lengo kuu la kuwepo Tanzania  ni kujenga uhusiano mzuri katika michezo husani mpira wa miguu kwa kuweka msingi mzuri wa kusaidia klabu za michezo na kukuza vipaji kwa vijana.
Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa Everton, Leon Osman amesema kuwa ni muhimu kuendeleza vipaji vya vijana ili kuweza kupata wachezaji mahiri.

Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii.

Mchezaji wa Zamani wa timu ya Everton ya Nchini Uingereza Leon Osman azindua programu ya timu za vijana nchini itakayosimamiwa na timu hiyo uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Osman aliyekuwa ameambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe walizindua programu hiyo kwa vijana wadogo ambapo itakuwa endelevu hapa nchini.
Akizungumza na watoto kutoka katika vituo mbalimbali vya kukuzia vipaji vya soka Osman amewataka kujituma zaidi ili waweze kufikia malengo yao.
Osman amewapatia zawadi ya mipira  vijana hao waliokuja na kuonyeshwa kufurahia namna wanavyojituma na kuonyesha vipaji vyao.
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zaman wa Everton Leon Osman (wa pili kulia) sambamba na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara Yusuph Singo (kulia) na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman (anayewasalimia vijana ) sambamba na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman akiwa uwanjani na baadhi ya vijana akiwapa maelekezo mbalimbali.
 Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman  akitoa zawadi ya mipira kwa vijana waliojitokeza katika uzinduzi wa programu hiyo itakayokuw aendelelevu chini ya Timu ya Everton.
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka vituo mbalimbali pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone.

Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa na mchezaji wa zaman wa Everton leon Osman (wa kwanza kushoto) sambamba na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara Yusuph Singo (kulia) na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone (wa nne kulia) na Mkurugenzi wa SportPesa Pavel Slavkov na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Sportpesa Tanzani Abbas Tarimba.

0 comments:

Post a Comment