NEWS ALERT; BOSS WA BARRICK GOLD AKUTANA NA RAIS MAGUFULI KATUBU NA KUKUBALI KUFANYA MAZUNGUMZO YA KULIPA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz...




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.
Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.
Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.
“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2017. Kulia ni balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Canada nchini Mhe Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa palamagamba kabudi akipeana mikono na Mwenyekiti wa  Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2017. Kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya mazungumzo yake na  Mwenyekiti wa Barrick  Gold Corporation ya Canada  (kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2017. Kulia ni Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Canada nchini Mhe Ian wakiwa na  Mwenyekiti wa  Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi  baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa  Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Barrick  Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2017. Pamoja nao ni Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles na  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Barrick  Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2017. (Picha na Ikulu)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NEWS ALERT; BOSS WA BARRICK GOLD AKUTANA NA RAIS MAGUFULI KATUBU NA KUKUBALI KUFANYA MAZUNGUMZO YA KULIPA
NEWS ALERT; BOSS WA BARRICK GOLD AKUTANA NA RAIS MAGUFULI KATUBU NA KUKUBALI KUFANYA MAZUNGUMZO YA KULIPA
https://lh4.googleusercontent.com/hSUMQj4XTP0yTSvlgMrQHp4-N5A0VfA43sHa26v1t1YwJ_hntEHv8fCDIPocJZnChOXsjdjJihz4EtnIgmrOuRHTFQfpmatHFHzTtgHhCPq7mpvEePqMExKbkZzIv-h9g2gYNJsDuHKQXbeF6w
https://lh4.googleusercontent.com/hSUMQj4XTP0yTSvlgMrQHp4-N5A0VfA43sHa26v1t1YwJ_hntEHv8fCDIPocJZnChOXsjdjJihz4EtnIgmrOuRHTFQfpmatHFHzTtgHhCPq7mpvEePqMExKbkZzIv-h9g2gYNJsDuHKQXbeF6w=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/news-alert-boss-wa-barrick-gold-akutana.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/news-alert-boss-wa-barrick-gold-akutana.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy