F NDUGAI AONGOZA WABUNGE KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA MJINI DODOMA | RobertOkanda

Sunday, June 18, 2017

NDUGAI AONGOZA WABUNGE KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA MJINI DODOMA


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, katika tukio lililofanyika Mjini Dodoma Juni 18 2017, Spika Ndugai pia alikuwa mgeni rasmi ambapo aliongoza Wabunge katika harambee hiyo. 
 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Pinda kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya Kikristo Tanzania, katika tukio lililofanyika Mjini Dodoma June 18 2017. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa. 

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiongoza Wabunge Mbalimbali kucheza nyimbo ya injili kama njia moja wapo ya kuhamasisha uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya Kikristo Tanzania, tukio lililofanyika Mjini Dodoma.
 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza jambo kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, tukio lililofanyika Mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa.
 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) baada ya kumalizika kwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, tukio lililofanyika Mjini Dodoma.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah baada ya kumalizika kwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, katikati ni Ndg. Elton Mapesa Mwakilishi wa Harambee kutoka External, Ubungo Jijini Dar es Salaam. Katika harambee hiyo, Spika wa Bunge, Mhe. Ndugai aliwaongoza wa Bunge katika uchangiaji wa ujenzi wa jengo hilo.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (wa pili kushoto) akizungumza jambo baada ya kumalizika kwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania. Kulia ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Askofu Dkt. Alex Malasusa (kushoto) na Elton Mapesa Mwakilishi wa Harambee kutoka External Ubungo Jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment