Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa rasmi wilaya ya Mkuranga ukitokea wilaya ya Rufiji huko mkoani Pwani na umetembelea miradi 11 ya Maendel...
Mwenge
wa Uhuru umekabidhiwa rasmi wilaya ya Mkuranga ukitokea wilaya ya
Rufiji huko mkoani Pwani na umetembelea miradi 11 ya Maendeleo yenye
thamani ya zaidi ya shilingi billion 24.7.
Akizungumza
wakati wa kubadhiwa mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Mkuranga,
Filibeto Sanga amesema miradi hiyo 11 iliyotembelewa ni pamoja na afya,
elimu, kilimo na mradi wa ujasilia Mali kwa vijana.
Aidha
katika miradi hiyo kumi na moja mwenge wa Uhuru umezindua miradi mitatu
ambayo ni huduma ya upasuaji katika kituo cha afya Kilimahewa, kufungua
nyumba za walimu katika shule ya sekondari Mkugilo pamoja na kuzindua
mradi wa maji katika kijiji cha Mwanambaya wilayani humo.
Kwa
upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 Amour
Hamadi Amour ametoa wito kwa watanzania kuwa na uzalendo wa kuthamini
vya kwao ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuifanya Tanzania ya
viwanda.
Kiongozi
huyo ameongeza kuwa katika kuelekea nchi ya viwanda ni vyema Watanzania
wakawa na utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wa
nchi na taifa kwa ujimla.
Hata
hivyo mbio hizo za mwenge wa Uhuru wilayani mkuranga mkoani Pwani
zimeudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Halmashauri hiyo akiwemo
Mkurugenzi injinia Mshamu Munde na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma
Abeid.
Mkuu
wa Wilaya ya mkuranga, Filibeto Sanga (kulia) akipokea mwenge wa uhuru
kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Abdalah tayari kwaajili ya
kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.mkoani Pwani.
Mganga
mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo wa (kwanza kulia) akitoa
maelekezo mbele ya viongozi wengine ya namna chumba upasuaji kitakavyo
saidia kinamama wajawazito kijiji cha kilomahewa.mkoani Pwani.
Kiongozi
Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akizindua
nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani.
Kiongozi
Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akipanda mti
katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani ikiwa ni ishara ya
kuhimiza wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira,
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid wa (kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Wilaya ya Mkuranga.
COMMENTS