Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mita...
Baadhi ya Watendaji wa Kata wakishangilia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielezea
lengo la mafunzo muda mchache kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe
Kisare Makori kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akifatilia kikao kabla ya kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori leo June 21, 2017 amefungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika
kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo kuhusu Mwongozo mpya
wa mapokezi na Matumizi ya fedha za LGDG (Local Government Development
Grant), Mpango wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O and OD-Oportunity
and Obstacle to Development), Rushwa mahala Pa kazi, Ulinzi na Usalama,
Na sheria ya Ardhi.
Mafunzo
hayo pia yatahusisha masuala ya Utawala bora, Majukumu ya Wenyeviti wa
Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa, Pia kujifunza kuhusu historia na
uhalali wa serikali za Mitaa, Sheria za uendeshaji wa Mamlaka za
serikali za Mitaa, Muundo, Madaraka na Majukumu ya serikali za Mitaa,
Mamlaka za serikali za Mitaa, Maadili ya viongozi wa Umma na Ulinzi na
usalama katika maeneo ya kazi.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe Makori alisema kuwa mafunzo hayo
yanayotolewa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa mafunzo
ulioidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kwa mwaka wa fedha
2016/2017.
Alimpongeza
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo kwa kuandaa
mafunzo hayo kwani yatatoa fursa kwa Wenyeviti na Watendaji wa Kata na
Mitaa kuimarika katika nidhamu ya utendaji hususani kutekeleza mambo
yaliyoainishwa kutekelezwa katika maeneo yao kwa maslahi ya wananchi.
Alisema
kuwa mafunzo hayo yatatoa ufanisi wa uelewa mipaka na mamlaka katika
utendaji jambo ambalo litawasaidia kuepuka migongano ya kimaslahi katika
utekelezaji wa shughuli za uwakilishi wa wananchi pamoja na kusimamia
utekelezaji wa shughuli za Halmashauri.
Aliongeza
kuwa mada zote ziatakazotolewa itakuwa ni chachu ya kufungua ukurasa
mpya kwa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kufuata miiko ya uongozi
na kuongeza uadilifu katika utendaji kazi wa kila siku ili kufikia
malengo yaliyoidhinishwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
alisema kuwa lengo la mafunzo hayo yanayotolewa kwa Wenyeviti wa Mitaa,
Watendaji Kata na Mitaa katika Manispaa ya Ubungo ni kuwajengea uwezo
katika kutatua matatizo ya wananchi, kuwasilisha mawazo yao katika vikao
vya kisheria, kuchambua sera na mikakati ya kutekeleza mipango
mbalimbali, kutafuta ufumbuzi wa changamoto za wananchi katika maeneo
yetu ya kusimamia majukumu yetu kikamilifu.
COMMENTS