MKUU WA WILAYA YA IKUNGI MHE MIRAJI MTATURU AFUTURISHA NA KUWASIHI WAISLAMU KUDUMISHA MISINGI YA QURAN

MKUU wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida  Miraji J. Mtaturu awafuturisha waislamu wa Wilaya hiyo huku akiwasihi kuendeleza tabia njem...


MKUU wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida  Miraji J. Mtaturu awafuturisha waislamu wa Wilaya hiyo huku akiwasihi kuendeleza tabia njema kwa kufuata misingi iliyohifadhiwa na Allah katika kitabu chake cha (Quran) hata baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan kumalizika.
Akizungumza na Waislamu hao baada ya kupata futuru Wilayani humo Mhe Mtaturu alisema kuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan watu wametenda mema yanayopaswa kuendelezwa hata baada ya mwezi huo.
"Wakati tupo kwenye mfungo huu tupo kwenye darasa la tabia njema hivyo nawashauri hata baada ya mfungo huu tuyaendeleze," alisema Mtaturu.
Alisema kuwa serikali inafarijika pale inapoona wananchi wake wakifuata imani za dini zao na hivyo kuwa raia wema na nchi kuendelea kuwa na amani.
"Tunamaliza kukamilisha moja ya nguzo tano za uislamu panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu, hivyo nawaombeni Ndugu zangu Waislamu hapa Wilayani Ikungi na Duniani kwa ujumla isiwe mwisho wa kufanya mema bali iwe ni mwendelezo wa kutenda haki, kudumisha amani na mshikamano katika siku zetu zote za maisha yetu," alisisitiza Mtaturu.
Mhe Mtaturu aliwatakia maandalizi mema ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akiwaasa kusherehekea kwa amani, utulivu na upendo na kukumbuka kutoa Zaka kwa watu wasio na uwezo.
Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumuombea Rais Dokta John Magufuli kutokana na kazi kubwa anayoifanya katika  kuendeleza  dhamira yake ya kulinda rasilimali za nchi ili ziwanufaishe watanzania wote hasa wale wanyonge na wasiojiweza.
Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya hiyo Abdi Seleman akitoa neno la shukrani alimshukuru mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwafuturisha na kusema kuwa hiyo ni mara ya kwanza toka wilaya hiyo ianzishwe kwa mkuu wa wilaya kuwaalika futari hivyo Mkuu huyo ameonyesha kuwajali watu anawaongoza.
"Kwa sadaka yako hii kwetu tunamuomba  Mwenyezi Mungu akulipe kila la kheri,na inshallah huu usiwe mwisho bali uwe mwanzo wa kufanya hivi," alisema Sheikh Seleman.
Nae Kadhi wa mkoa wa Singida Ramadhan Kaoja alimshukuru  mkuu wa wilaya hiyo na kusema hiyo ni dalili za kiongozi bora kwa kuwa karibu na jamii lakini pia ni sehemu ya kukamilisha imani yake ambapo kwa mwezi huu wa Ramadhan kwa kufuturisha anapata thawabu nyingi sana.
Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya IkungiMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akihutubia mamia ya wakazi wa Wilaya hiyo waliojitokeza wakati wa futari katika Ukumbi was Shule ya Sekondari Ikungi.Kadhi wa mkoa wa Singida Ramadhan Shekh Kaoja akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya waumini wote waliojitokeza kwenye ibada ya futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. MtaturuMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akihutubia mamia ya wakazi wa Wilaya hiyo waliojitokeza wakati wa futari katika Ukumbi was Shule ya Sekondari IkungiMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kushoto) Akimshukuru mwenyekiti wa CCM wilaya Ndg Hassan Tati kwa kuhudhuria hafla ya futari katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari IkungiMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kushoto) Akimshukuru Kadhi wa mkoa wa Singida Shekh Ramadhan Kaoja kwa kuhudhuria hafla ya futari katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari IkungiWaumini wakimpa mkono Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu mara baada ya hafla ya futari aliyowaandalia katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi kukamilika.Waumini wakimsikiliza kwa making Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu mara baada ya hafla ya futari aliyowaandalia katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi kukamilika.Waumini wakimsikiliza kwa making Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu mara baada ya hafla ya futari aliyowaandalia katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi kukamilikaWaumini wakimsikiliza kwa making Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu mara baada ya hafla ya futari aliyowaandalia katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi kukamilika

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUU WA WILAYA YA IKUNGI MHE MIRAJI MTATURU AFUTURISHA NA KUWASIHI WAISLAMU KUDUMISHA MISINGI YA QURAN
MKUU WA WILAYA YA IKUNGI MHE MIRAJI MTATURU AFUTURISHA NA KUWASIHI WAISLAMU KUDUMISHA MISINGI YA QURAN
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2t3-DL5D_32EWQh1yh51cX1-uvzXOK2llNsfnLP2SiADhmTCeGC_ayMwbzmCK729neThpFoadalcFnr2UfafHjlIgx-H1iX7sFo8uqkSMaox9ByObBCWH3aqkbC2N9v3LG_-QDcNtRr8/s640/IMG-20170625-WA0011.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2t3-DL5D_32EWQh1yh51cX1-uvzXOK2llNsfnLP2SiADhmTCeGC_ayMwbzmCK729neThpFoadalcFnr2UfafHjlIgx-H1iX7sFo8uqkSMaox9ByObBCWH3aqkbC2N9v3LG_-QDcNtRr8/s72-c/IMG-20170625-WA0011.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mkuu-wa-wilaya-ya-ikungi-mhe-miraji.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mkuu-wa-wilaya-ya-ikungi-mhe-miraji.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy