MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI WAKAMILISHWA.

Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUP) Dkt. Stephen Nindi akizungumza kwa ufupi hatua iliyofika kabla...



Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUP) Dkt. Stephen Nindi akizungumza kwa ufupi hatua iliyofika kabla ya kwenda kukabidhi rasimu hiyo katika vyombo vya juu


Mkurugenzi msaidizi nyanda za malisho kutoka wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Victor Mwita (kulia) ambaye alikuwa mwenyekiti wakati wa shughuli hiyo, akitoa mwongozo wa baadhi ya mambo.
Baadhi ya watumishi Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUP) wakiwa wanafuatilia kwa makini majadiliano hayo wakiwa mkoani Morogoro.
Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho akichangia jambo wakati wa mjadala
Amina Ndiko kutoka Shirika la kimataifa la Oxfam nchini Tanzania akitoa neno la shukurani mara baada ya kukamilisha zoezi la kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi.
Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care, Mary Ndaro akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo changamoto kubwa iliyopo inayochangia ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo
Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Misitu na Nyuki akichangia jambo wakati wa kukamilisha mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi
Kikosi kazi wakiendelea na kazi ya majumuisho
Zakaria Faustin Mratibu wa kitengo cha Ardhi  na uwekezaji kutoka (TNRF) akizungumza jambo wakati wa majumuisho hayo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikosi kazi



Kikosi Kazi cha Masuala ya Matumizi ya Ardhi kinachojumuisha wadau kutoka serikalini na asasi za kiraia wamekutana na kukamilisha rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya ardhi
nchini.
Mkakati itakayowasilishwa katika ngazi ya juu endapo utatekelezwa ,kusimamiwa na kufatiliwa kwa umakini kwa asilimia kubwa nchi ya
Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zenye utulivu wa migogoro ya ardhi




Miongoni mwa wadau hao waliohudhuria katika kikao wapo kutoka taasisi za serikali na zisizo za serikali ikiwemo  Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya
Ardhi (NLUP), Shirika la kimataifa la Care pamoja Shirika la Oxfam.

Akizungumza  Mkoani Morogoro, Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUP)
Dkt. Stephen Nindi alisema  endapo rasimu hiyo itapitishwa na yale yaliyokuwepo ndani ya rasimu
yakasimamiwa na kufatiliwa vizuri kwa kiasi kikubwa itawezesha vijiji na Wilaya kuwa na mpango mzuri wa  matumizi bora
ya Ardhi.

“Ndani ya rasimu hiyo imeweza kuchambua vizuri suala zima la matumizi ya Ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa itaondoa na kumaliza  tatizo la migogoro ya ardhi katika maeneo mengi ya nchi, baada ya rasimu hiyo kukamilika itaweza kupelekwa katika ngazi ya juu kwa  ajili ya kupewa baraka na kuanza utekelezaji wake.” Alisema Dkt. Nindi Alisema kuwa kikosi kazi hicho kimeweza kutengeneza mipango ya ardhi takribani 100 kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kikosi kazi hicho
kipipo undwa.

"Ile kazi ambayo tuliifanya kipindi kirefu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka Serikali na taasisi zisizo za  kiserikali  tangu mwaka jana kwa sasa imefikia katika hatua ya mwisho ya  kuwasilishwa katika vyombo vya juu kwa lengo la  kupewa baraka ili utekelezaji wa jambo hilo liweze kuanza ,"alisema Dkt Nindi

Nae Mratibu wa programu ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Care  Bi. Mary Ndaro alisema kuwa lengo kubwa la wao kukutana na wadau mbalimbali wa mipango ya matumizi bora ya ardhi ni pamoja na kuhakikisha kuwa kuna kasi ya upangaji wa ardhi katika nchi.

"Moja ya changamoto kubwa iliyopo inayochangia ucheleweshaji wa upimaji wa ardhi ni pamoja na kuwepo kwa bajeti ndogo. Maeneo mengi yakipimwa yanasaidia kuwepo kwa usalama wa miliki na hati miliki hususani kwa wananchi wa vijijini  ambapo karibia asilimia 60 ya wananchi wanategemea ardhi kwa ajili ya kujipatia kipato hivyo kama nchi ni vema kuwekeza katika upangaji wa matumizi ya ardhi ili kusaidia kupunguza migogoro
ya ardhi,”alisema Ndaro
 


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI WAKAMILISHWA.
MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI WAKAMILISHWA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPgxTnhSVSvxOexSltuBYVAyvPSqpQoYTuRuzPqlHOFkIGqn8TOcIJcdRKEMldyTMrqI0r0xq5IAP7NfGc8ttC7FMjnvkXrO48S0n7o823TtklM8XePTno0mxURfpie4EzDv6gGEFu6CUC/s640/22.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPgxTnhSVSvxOexSltuBYVAyvPSqpQoYTuRuzPqlHOFkIGqn8TOcIJcdRKEMldyTMrqI0r0xq5IAP7NfGc8ttC7FMjnvkXrO48S0n7o823TtklM8XePTno0mxURfpie4EzDv6gGEFu6CUC/s72-c/22.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mkakati-wa-kukabiliana-na-changamoto-za.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/mkakati-wa-kukabiliana-na-changamoto-za.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy