MASALIA YA MIJUSI MIKUBWA KUTORUDISHWA NCHINI

Na Mwandishi Wetu Wazo la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama ikilinganishwa na faida z...

Na Mwandishi Wetu
Wazo la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo.
Akijibu swali la Mbunge wa Mchinga Mhe. Hamidu Hassan Bobali lililo uliza, ni nini kauli ya mwisho ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wananufaika kutokana na mabaki hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza kupata manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujerumani.

Joka wa Komodo ni mjusi mkubwa kabisa

“Kufuatia majadiliano ya kina yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Mali Kale kutoka pande zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha shughuli za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika maeneo hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za Utalii zifanyike katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi” alisisitiza Mhe. Makani.
Kuhusu Serikali kupunjwa mapato yatokanayo na viingilio katika Makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin, Mhandisi Makani amesema jambo hilo halina ukweli wowote kwani ni ngumu kufahamu ni kiasi gani hupatikana kama kiingilio kuwaona Mijusi kutoka Tanzania kwakuwa Makumbusho hiyo ina kumbi nyingi zenye masalia kutoka nchi mbali mbali za Afrika na gharama za kuendesha Makumbusho hiyo hutolewa na Serikali ya Ujerumani.
Ameeleza kuwa Serikali ya Ujerumani itafadhili zoezi la uimarishaji idara inayohusika na Malikale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wa kutosha wa fani husika ilikuendeleza Utalii wa Malikale nchini.

Huyu ni mjusi aina ya Gwancko Williamsiis kwa jina la Kitaalamu huku wenyeji wanamuita Mabagalaja.

Mijusi mikubwa (Dinosaria) ilichimbwa katika Kilima cha Tendaguru, mkoani Lindi kati ya waka 1909 na mwaka 1913 na kupelekwa katika makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin nchini Ujerumani.





COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MASALIA YA MIJUSI MIKUBWA KUTORUDISHWA NCHINI
MASALIA YA MIJUSI MIKUBWA KUTORUDISHWA NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgRCxmaSKAN6J8rBbYRAvY7cVsqi8mK_n2cIUr2-CXheMTgso2huTcgH_ODdESvA6MxfrnyPE1TW2rk6T9yaSLHoBnJaDy2ojFbPR-8d08msPIs57xX18Ok1VCt5KPIS5cDyRUicOcpd-4/s640/Komodo+aliyepumzika.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgRCxmaSKAN6J8rBbYRAvY7cVsqi8mK_n2cIUr2-CXheMTgso2huTcgH_ODdESvA6MxfrnyPE1TW2rk6T9yaSLHoBnJaDy2ojFbPR-8d08msPIs57xX18Ok1VCt5KPIS5cDyRUicOcpd-4/s72-c/Komodo+aliyepumzika.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/masalia-ya-mijusi-mikubwa-kutorudishwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/masalia-ya-mijusi-mikubwa-kutorudishwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy