Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa ...
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina
mama wajawazito wakati na baada ya kujifungua vilivyotolewa na Shirika
la Red Crescent la Kuwait ambapo mabeseni 100 yenye vifaa hivyo kati ya
1000 yalikabidhiwa kwa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, Dar es Salaam.
Balozi
wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akihutubia mbele ya Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa
zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati
kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo
zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na
Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye
vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho
kilipokea mabeseni 100.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa
zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati
kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo
zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na
Zanzibar, hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye
vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho
kilipokea mabeseni 100, Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya mabeseni yenye vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu
Hassan pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakiangalia mbabeseni
yanya vifaa vya kusaidia wakina mama kujifungua yaliotolewa na Shirika
la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa
hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3
ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha
Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Bi.Arafa Nurdin wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya
hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa
vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Mbagala Rangi Dkt. Joseph Kiani wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya
hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa
vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimsalimia mtoto mwenye miezi miwili Jenifer Mathias, kulia ni
baba wa mtoto Bw. Mathias Miano mkazi wa Kingugi, Mbagala kabla uzinduzi
wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati
kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo
zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na
Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye
vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho
kilipokea mabeseni 100
Sehemu
ya wananchi wa Mbagala Kizuiani kwenye kituo cha Afya cha Mbagala Round
Table waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa zoezi la
kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua
Juni20 2017. Vifaa hivyo vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya
mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar.
..............................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua
zoezi la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 200 yaliyotolewa na
Ubalozi wa Kuwait nchini kwa ajili ya wanawake wajawazito katika
hospitali ya Mbagala Rangi Tatu na Kituo cha Afya cha Mbagala Round
Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Lengo
la mpango huo ni kutoa mabeseni hayo zaidi ya 1,000 kwa wanawake
wajawazito wasio na uwezo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kama
hatua ya kukabiliana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito nchini.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa tiba hivyo, Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa
mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupambana na vifo vya
watoto na wanawake wajawazito kwa kukosa vifaa tiba kutokana na umaskini
unaowakabili.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa maeneo yaliyopatiwa
mabeseni yenye vifaa tiba yahakikishe vifaa hivyo vinatolewa kwa
wanawake wajawazito ambao baadhi yao wanakata tamaa kwenda kujifungulia
kwenye hospitali au kwenye vituo vya afya kwa kukosa vifaa hivyo kwa
sababu ya umaskini.
Amesema
mkakati uliopo wa Serikali ni kuhakikisha huduma za afya nchini
zinaendelea kuboreshwa hasa huduma ya mama na mtoto ambapo kutokana na
umuhimu wa sekta ya afya Serikali imetenga fedha za kutoka katika bajeti
ya mwaka 2017/2018.
Makamu
wa Rais ameeleza kuwa mradi huo wa ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba
katika mradi huo kuanzia sasa utasimamia na wake wa viongozi wastaafu
na wakiwemo wake wa mawaziri baada ya kuuzindua rasmi.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa
msaada wake huo ambao amesema utakuwa ni chachu ya kupambana na vifo vya
watoto na wanawake wajawazito Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa
upande wake, Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesema
Serikali ya Kuwait kupitia kwa Jumuiya ya Red Crescent ya nchini hiyo
itaendelea kusaidia vifaa tiba mbalimbali kwa upande wa Tanzania Bara na
Zanzibar ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu
na maeneo yao.
Balozi
huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesisitiza kuwa milango ya
ubalozi wa Kuwait ipo wazi kwa Taasisi mbalimbali za Kiserikali kupeleka
maandiko mbalimbali kwa ajili ya kuomba kupatiwa misaada lengo likiwa
ni kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma za viwango vya juu
katika sekta mbalimbali.
Amesema
kwa sasa Serikali ya Kuwait ipo mbioni kutiliana saini ya makubaliano
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kufanya ukarabati
mkubwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo Unguja.
Ameeleza kuwa ukarabati huo utaiwezesha hospitali hiyo kuongeza utoaji wa huduma bora kwa wananchi wengi zaidi.
Halfa
ya makabidhiano ya mabeseni 200 ya vifaa tiba katika hospitali ya
Mbagala Rangi Tatu na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika
wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi
mbalimbali ikiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
COMMENTS