MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA TAARIFA YA THBUB KWA VYOMBO VYA HABARI

- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 213...


-
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Tovuti: www.chragg.go.tz

Juni 16, 2017
   
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, 2017

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za watoto duniani katika kuadhimisha “Siku ya mtoto wa Afrika”. Siku hii inaikumbusha dunia juu ya mauaji ya watoto wapatao 2,000 wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini, waliouawa kikatili miaka 41 iliyopita na iliyokuwa Serikali ya Makaburu.

Siku hii ilizinduliwa rasmi mwaka 1991 na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ili kuwakumbuka watoto hao waliokuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za binadamu.

Wakati tunaadhimisha siku hii muhimu wadau wote wa haki za watoto hatuna budi kujitathimini namna tunavyowaandaa watoto wetu ili waweze kutoa mchango stahiki katika maendeleo ya taifa letu, kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema: “Maendeleo endelevu 2030: Imarisha ulinzi na fursa kwa watoto wote.”

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizochukua hatua mbalimbali kuhakikisha uwepo wa maslahi ya watoto. Hatua hizo ni pamoja na kutunga sheria na kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda inayolinda na kutetea haki za mtoto. Mikataba hiyo inajumuisha: Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto (1989), Tamko la Shirika la Kazi Duniani (ILO) Na. 182, na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (2003).

Miongoni mwa sheria zilizotungwa katika ngazi ya kitaifa ni: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), Sheria ya Mtoto Na. 21/2009, Sheria ya Kanuni za Adhabu, Sheria  ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).

Pia imeridhia na kubuni sera, mipango na mikakati mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo: Sera ya Mtoto (2008), na Mpango-kazi wa Kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017- 2022).

Kimataifa imeridhia na inatekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDG’s) yaliyopitishwa mwaka 2015 yanayobainisha kuwa watoto wana haki ya kuishi, kulindwa, kutobaguliwa na kushirikishwa kwa usawa ili kuhakikisha kuwa wanapata fursa sawa katika jamii.

Ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kinara wa kujali haki za watoto Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia imeanzisha taasisi na vyombo mbalimbali vinavyoshughulikia ulinzi na ukuzaji wa haki za watoto nchini. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni miongoni mwa taasisi hizo.

Tume imekuwa ikitoa elimu ya haki za binadamu, ikiwemo haki za watoto kupitia vyombo vya habari, semina na mikutano  mashuleni na maeneo mbalimbali inayopata fursa ya kuyafikia.

Pia, Tume imekuwa ikitoa huduma za kisheria kwa makundi yenye uhitaji ambao ni pamoja na watoto na watu wengine wenye uhitaji wa msaada wa kisheria na pia imeanzisha dawati mahsusi linaloshughulikia haki za watoto.

Vilevile, Tume imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa haki za binadamu kimataifa na kitaifa ili kuweka nguvu ya pamoja katika kulinda haki za binadamu na kukemea vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi yao.

Aidha, kupitia Mpango-kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu (National Human Rights Action Plan - 2013-2017) Tume imefanikiwa kutoa mafunzo kwa waalimu na watendaji wengine katika sekta ya elimu na kuhamasisha uanzishwaji wa vilabu takriban 130 vya haki za binadamu shuleni. Pamoja na mambo mengine vilabu hivi vinajihusisha na utoaji wa elimu ya haki za binadamu ikiwemo elimu ya haki za watoto, shuleni na nje ya shule.

Juhudi hizo ni muhimu kipindi hiki katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia azma yake ya “Kujenga Tanzania ya Viwanda.”

Pamoja na jitihada hizi zote bado zipo changamoto mbalimbali zinazoathiri malezi ya watoto na kuwanyima fursa katika jamii, changamoto hizo ni pamoja na: umaskini, migogoro ya wanandoa, mila potofu, utandawazi, majukumu ya kijinsia katika jamii na ukosefu wa haki ya elimu ya afya ya uzazi (reproductive and health rights).
Tume inaitaka jamii kuwapa umuhimu watoto wa kike na kuachana na mtazamo potofu kuwa hawana mchango mkubwa kwa jamii, hali inayochangia utumikishwaji wa watoto na kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na biashara ya ngono katika umri mdogo.

Vitendo hivyo vimekuwa chanzo cha mimba na ndoa za utotoni ambazo huwaletea madhara mbalimbali ikiwemo: unyanyasaji wa kimwili, kisaikolojia, kingono, athari za kiafya, vifo wakati wa ujauzito/kujifungua na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU).

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) mwaka 2014, tatizo la ndoa za utotoni lipo duniani kote. Takriban wasichana milioni 15 wanaolewa kila mwaka chini ya umri wa miaka 18. Ikiwa ni wastani wa watoto wa kike 41,000 kwa siku.

Utafiti huo ulibaini kuwa tatizo la mimba za utotoni kwa Tanzania ni kubwa, ambapo wasichana 4 kati ya 10 (sawa na asilimia 40) wanaolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Pia kwa mujibu wa takwimu za demografia ya afya Tanzania (TDHS, 2016) asilimia 36 ya wanawake wa kitanzania wenye umri wa miaka kati ya 20-24 waliolewa au waliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa mara ya kwanza kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Watoto Duniani (UNICEF, 2012) zimeitaja Mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni kuwa ni: Mkoa wa Shinyanga ukiongoza kwa asilimia 59. Ikifuatiwa na Tabora (58%), Mara (55%), Dodoma (51%) na Lindi (48%).

Hivyo basi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapendekeza na kutoa wito kama ifuatavyo:
  1. Serikali ifanye marekebisho ya sheria kandamizi na zinazopingana na sheria zingine. Mfano;- Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inaweka miaka 18 kuwa umri mdogo ambao wavulana wanaruhusiwa kuoa, lakini imeweka umri wa miaka 15 kwa wasichana kuolewa kwa ridhaa ya wazazi.

  1. Mamlaka zinazotoa haki kwa wahanga wa ukatili, wakiwemo watoto zitoe haki kwa wakati.

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ihakikishe uwepo wa mfumo utakaowawezesha watoto wa kike wanaopata mimba mashuleni kuendelea na masomo yao mara tu wanapojifungua.

  1. Wadau wa haki za binadamu waendelee kutoa elimu ya haki za binadamu kwa jamii, ili kubadili mila na tamaduni potofu. Pia kukemea vitendo vya ukatili, unyanyasaji na udhalilishaji wa watoto.
  1. Wazazi wawajibike katika malezi ya watoto ili kuimarisha familia zao na kuwaepusha na viashiria hatarishi kwa maisha ya watoto wao.

  1. Watoto wapatiwe elimu ya afya ya uzazi ili waweze kujitambua na kuwa na uelewa juu ya madhara ya mimba na ndoa za utotoni.

  1. Wadau mbalimbali wa haki za watoto kuhakikisha kuwa ulinzi, usalama na haki za mtoto vinaimarishwa. Aidha, wahakikishe watoto wa kike na wa kiume wanapatiwa malezi bora yanayotoa fursa sawa kwa wote ili kuhakikisha kuwa ndoto zao katika maisha zinafikiwa.

  1. Wadau wote wa haki za binadamu kuhakikisha kuwa kama taifa tunaondoa aina zote za ukatili na ubaguzi dhidi ya watoto na kuwapa haki na fursa sawa katika umiliki wa rasilimali na nyanja zote za kimaisha na kusimamia Sheria na Sera zinazolinda usawa wa kijinsia ili taifa letu liweze kufanikisha lengo la fursa sawa kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Imetolewa na:
(SIGNED)

Salma Ali Hassan
(Kamishna)

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Juni 16, 2017.
 
Salma Ali Hassan (Kamishna)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA TAARIFA YA THBUB KWA VYOMBO VYA HABARI
MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA TAARIFA YA THBUB KWA VYOMBO VYA HABARI
https://lh5.googleusercontent.com/JyoejT_bopT4e3X8drs5cf4Td6aumO5ZQgxnlMokAuYjGWuSbFo6XibY2cEkCrXWdYI0Dq30l_uZsPIqqOi24RI_7AdHWU7-M23WVRWSix9viD8GAhGTuc3uTuQK-06zGZbLtzrHFdNMPJtnEA
https://lh5.googleusercontent.com/JyoejT_bopT4e3X8drs5cf4Td6aumO5ZQgxnlMokAuYjGWuSbFo6XibY2cEkCrXWdYI0Dq30l_uZsPIqqOi24RI_7AdHWU7-M23WVRWSix9viD8GAhGTuc3uTuQK-06zGZbLtzrHFdNMPJtnEA=s72-c
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/maadhimisho-ya-siku-ya-mtoto-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/maadhimisho-ya-siku-ya-mtoto-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy