KONGAMANO LA PILI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAFANYIKA MKOANI DODOMA

  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaj...


 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika Juni 10 mjini Dodoma. TSN walikuwa mmoja wa wadhamini. Dk Yonazi alisema kuwa ili kuwaezesha wananchi kiuchumi ni lazima jamii ihabarishwe juu ya fursa mbalimbali zilizopo, lakini pia muhimu wa sekta binafsi kuwa na ubunifu na mifumo ya kujitengenezea utajiri. (Picha zote na Mroki Mroki-dailynewstzonline.blog)


Afisa Mtendaji Mkuu wa MM Maxcom, Engineer Juma Rajab akielezea uzoefu wake na kusema kuwa inahitajika kuwawezesha wajasiriamali wote, wadogo, wa kati na wakubwa ili kufanikisha wananchi kuweza kuingia katika uchumi wa viwanda.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa mada juu ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo alisema ni vyema viongozi na jamii ikawana na utaratibu wa kuchapa kazi ili iweze kufanikiwa katika suala la uwezeshaji
wananchi kiuchumi.


 Wakuu wa Mikoa waliohudhuria Kongamano hilo.
 Wadau wa Kongamano hilo kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) nao walikuwepo. TSN ilikuwa moja ya wadhamini.
 washiriki wa Kongamano
 Wakuu wa Mikoa Mbeya, Amos Makala (kulia) na John Mongela wakifuatilia kongamano hilo. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.


 Dk. John Kyaruzi kutoka SAGGOT CTF akitoa mada na kuwelka wazi kuwa taasisi hiyo iko vizuri kuwawezesha wananchi. Aidha alisema ni vyema sasa wananchi wakalazimishwa kulima kibiashara tofauti na ilivyo sasa.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Sera na Utafiti wa TPSF,Gili Teri akizungumza katika kongamano hilo na kuitaka Serikali iweke mazingira wezeshi ya uhakika na halisi kwa sekta binafsi ili ishiriki katika kukuza uchumi.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika kongamano hilo.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa akizungumza na kuelezea Malego ya Kongamano hilo.
 Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Amos Makala akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna
Mghwira walipokutana katika Kongamano la pili la  Uwezeshaji wananchi Kiuchumi mjini Dodoma.
 Dk.
John Kyaruzi kutoka SAGGOT CTF akitoa mada na kuwelka wazi kuwa taasisi
hiyo iko vizuri kuwawezesha wananchi. Aidha alisema ni vyema sasa
wananchi wakalazimishwa kulima kibiashara tofauti na ilivyo sasa.
 Msimamizi wa Mijadala katika Kongamano hilo, Profesa Honest Ngowi akiongoza wawezeshaji.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa akifuatilia mijadala.
 Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini kutoka kwa wawezeshaji wabobevu.

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (MB), akichangia mada wakati wa Kongamano la Pili la Uwezeshaji wananchi kiuchumi lililofanyikajana mjini Dodoma chini ya uandaa wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)kuwa mmoja wa wadhamini.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula akichangia mada wakati wa Kongamano la Pili la Uwezeshaji wananchi kiuchumi lililofanyika jana mjini Dodoma chini ya uandaa wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa mmoja wa wadhamini. 
 Wawezeshaji wakifuatilia mada
 Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi akizungumza katika kongamano hilo.
 Mmoja wa washiriki akiuliza swali juu ya namna vijana wanavyowezeshwa kushiriki katika Uchumi wa viwanda hasa katika sekta ya Kilimo.
 Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADP), Francis Assenga akizungumza na kuweka wazi namna TADP inavyoweza kusaidia miradi mbalimbali hasa katika kilimo. 





Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jana mjini Dodoma wengine meza kuuni wawezeshaji katika kongamano hilo. TSNwalikuwa  mmoja wa wadhamini.


 Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
 Jopo zima la wawezeshaji likiongozwa na Profesa Honest Ngowi (wanne kulia) likiwa meza kuu.
 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wakiwa katika Kongamano hilo.
Washiriki kutoka kada mbalimbali.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KONGAMANO LA PILI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAFANYIKA MKOANI DODOMA
KONGAMANO LA PILI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAFANYIKA MKOANI DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEio01tw7h_Jq7RXyv4Zj_Tk6z9-xsWbuMNBbN_253VN1r7yp-1tLDyGEUf9OvzDaJLeZj1VYTuSWeO1w7vFI6ABE1_gMBqjaMvF7KmRdD5AID1gDCA6Y0_bcAGCQelrnN43_TxWPKXy5Row/s640/6.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEio01tw7h_Jq7RXyv4Zj_Tk6z9-xsWbuMNBbN_253VN1r7yp-1tLDyGEUf9OvzDaJLeZj1VYTuSWeO1w7vFI6ABE1_gMBqjaMvF7KmRdD5AID1gDCA6Y0_bcAGCQelrnN43_TxWPKXy5Row/s72-c/6.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kongamano-la-pili-la-uwezeshaji.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kongamano-la-pili-la-uwezeshaji.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy