KILIMANJARO DIALOGUE INSTITUTE YAENDESHA MDAHALO WA MAZINGIRA MANISPAA YA ILALA

Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi.Esther Masomhe, (kulia), akizungumza jambo wakati wa mazungumzo ya mez...






Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi.Esther Masomhe, (kulia), akizungumza jambo wakati wa mazungumzo ya meza ya duara kuhusu mazingira kwenye Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Juni 5, 2017, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute iliyoandaa majadiliano hayo, Habib Miradji.







NA KVIS BLOG/Khalfan Said
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema iko kwenye mkakati mkubwa wa kutengeneza bustani za kupumzika wananchi na tayari wameanza kuboresha maeneo hayo kwa
kuanzia na eneo bustani ya Samora (Kaburi la Sharif), barabara ya Samora.
Akizungumza kwenye mdahalo wa mazingira uliotayarishwa na Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute ya jijini Dar es Salaam leo Juni 5, 2017, Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo, Esther Masomhe, alisema, pamoja na vipaumbele vingi ambavyo Manispaa hiyo inakabiliwa navyo, lakini moja ya hatua inazochukua ni kupendezesha jiji, (City beatification).
“Kuna maeneo tayari tumeanza nayo kama vile bustani ya Samora pale kaburi la Shariff, barabara ya Samora, bustani ya Mnazi Mmoja namba mbili eneo laMcahfukoge, tunakusudia kuiboresha bustani hiyo ili wananchi wapate mahala pazuri pa
kupumzika.” Alisema Bi.Masomhe.
Akifafanua zaidi alisema, Wilaya ya Ilala ndiyo kitovu cha jiji la Dar es Salaam hivyo Manispaa inachukuajuhudi mbalimbali kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa katika
muonekano mzuri kwa kuboresha mazingira na bustani zake.
Aidha Afisa huyo wa Mazingira wa wilaya ya Ilala alisema, kwa kuzingatia kauli mbiu
ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, ““Hifadhi Mazingira, kama Muhimili wa Maendeleo ya Viwanda
“kauli mbiu hii ina maana kuwa viwanda vingi hapa nchini vimejengwa bila kuzingatia uhifadhi wa mazingira, utakuta mtu mwenye kiwanda, anashindwa kuhifadhi maji
taka anayozalisha na badala yake anatiririsha kwenye mito, ambako huko kuna viumbe hai, sihilo tu lakini pia kuna watu wanaendesha kilimo cha mboga mboga, kwa vile maji wanayotumia ni hayo hayo ya mto ambayo tayari yanakuwa yamechanganyika na maji taka ya viwandani, walima bustani hutumia maji hayo
kunyweshea bustani zao na hivyo kuwalisha wananchi mboga mboga zenye kemikali na hii ni hatari kwa afya,” alisema
Alisema kwa kuwa sheria zipo wazi, watasimamia sheriahizo kikamilifu ili kuhakkiikisha kiwanda kitakachoanzishwa kwenye Manispaa knazingatia uhifadhi wa mazingira.
Naye Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya Kilimanjaro Dialogue Institute, Habib Miradji amesema, “hakuna mtu ambaye
hafahamu umuhimu wa mazingira, lakini kumekuwepo na tatizo kubwa la kimazingira, sisi tunaetembea dunia tunaona kuna milima misitu ya asili na mbuga, kwa kweli inabidi ukae ufikirie jinsi maliasili ilivyotunzwa, lakini hapa kwetu, vitu kama hivi havipo, ilikuwa zamani tu maana hata milio ya ndege na
miti asili imetoweka.” Alisema.
Bw. Miradji alihoji nini mikakati ya Manispaa katika uhifadhi wa mazingira kwani maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu hususan uswahilini, (Urban slams) haya yanakuwa na ongezeko la watu kwa haraka, familia moja inawezakuwa na watu 10 na zaidi, nini mkakati ya Manispaa
katika kukabiliana na misongamano ya watu?
Akijibu hoja hiyo Bi. Masomhe alisema, kumekuwepo na mikakati mbalimbali ikiwemo ya utoaji elimu mashuleni, kupitia klabu za mazingira za shule, lakini pia kuboresha miundombinu kwenye maeneo hayo na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo
hayo kupitia kwa maafisa afya wa Manispaa ambao hutembelea mara kwa mara ili kutoa elimu ya usafi wa mazingira.


 Esther Masomhe, akizungumzia mikakati ya Manispaa yake kuhusu mazingira na utunzaji wake
 Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Habib Miradji


 Mshauri wa masuala ya vyombo vya habari, Felix Kaiza akisikiliza kwa makini mjadala huo.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Hassan Mzighani (kulia), akizungumza kwenye mdahalo huo ambapo alisema anasikitishwa na jinsi Manispaa inavyoshindwa kudhibiti maji taka, yakiwemo yale yanayosababishwa na
mvua na kutolea mfano nchi kama Norway, ambayo hupata mvua muda mwingi lakini sio rahisi kukuta barabara au makazi ya watu yakiwa yamezingirwa na maji.




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KILIMANJARO DIALOGUE INSTITUTE YAENDESHA MDAHALO WA MAZINGIRA MANISPAA YA ILALA
KILIMANJARO DIALOGUE INSTITUTE YAENDESHA MDAHALO WA MAZINGIRA MANISPAA YA ILALA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9KuDLGsQ46yfISkVxzj7DW2CzDnb57bnn8lVUTkgKn48QjpIE4VWkCKkDOfHO_8AifMJNnjH9xBD2Nu-gTZJ3DQWh7CiFmI16cIomOKy7bVQVRKd0319I_aqKP9Dy54h0wwRILvfHEKI/s640/5R5A4795.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9KuDLGsQ46yfISkVxzj7DW2CzDnb57bnn8lVUTkgKn48QjpIE4VWkCKkDOfHO_8AifMJNnjH9xBD2Nu-gTZJ3DQWh7CiFmI16cIomOKy7bVQVRKd0319I_aqKP9Dy54h0wwRILvfHEKI/s72-c/5R5A4795.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kilimanjaro-dialogue-institute.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kilimanjaro-dialogue-institute.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy