Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya awali ya ufunguzi ...
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akitoa maelezo ya awali ya ufunguzi katika mijadala ya
kuadhimisha siku Mazingira Duniani Wilayani Butiama Mkoni Mara. Kauli
mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”
Wanajopo
wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka
kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi
Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi
Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in
Tanzania). Mjadala unaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya
Mazingira Duniani.
Mjadala
ukiendelelea pichani, Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa
na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack
Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos
Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS), Bi. Maria Sarungi (Mwendesha Mada) na Eng. Estomih Sawe
Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy
Initiative in Tanzania). Kongamano linaendelea Butiama katika
kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba akifuatilia
mjadala katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Butiama- Mara. Wapili kushoto
ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Mijadala
mbalimbali inaendelea katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na
Mazingira.”
COMMENTS