KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO DKT. TITO MWINUKA AWAHAKIKISHIA WATANZANIA MRADI WA UMEME WA GESI ASILIA WA KINYEREZI II UNAENDELEA KWA KASI

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na  Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, M...






Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na  Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi Simon Jilima (kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere, wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.




NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO), limewahakikishia watanzania kuwa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika kama ilivyopangwa.

Hakikisho hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka,
wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240 za umeme.
“Niwahakikishie Watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi II utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.” Alisema Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
Dkt. Mwinuka alifuatana na wakurugenzi watendaji wasaidizi, Mhandisi Abdallah O.
Ikwasa, (anayeshughulikia Uzalishaji), Mhandisi Khalidi James,
(anayeshughulikia uwekezaji miradi) na Mhandisi Kahitwa Bishaija (anayeshughulikia Usambazaji).
Dkt. Mwinuka alisema watanzania wanahitaji umeme ulio wa uhakika na kwamba Serikali
kupitia TANESCO imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa
watanzania na hivyo kuchangia pato la taifa.

“Kama mjuavyo serikali imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha Shirika linatekeleza
miradi hii na tayari shilingi Bilioni 110 zimetolewa na serikali katika kutekeleza mradi huu wa Kinyerezi II.” Alifafanua Dkt. Mwinuka.

Awali Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephens S.A.Manda, alisema, wataanza kuingiza
umeme kwenye gridi ya taifa kila mwezi kuanzia Disemba mwaka huu 2017 ambapo
Megawati 30 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa.

“Tuna mashine 8 ambazo zitafua umeme huo kwa hiyo kuanzia Disemba Mosi mwaka huu, tutaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na tutafanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja
kwani tunaelewa kuwa serikali ambayo imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda,
tunaona umeme ni hitajio muhimu kwa hivyo kila tutakapokamilisha mtambo mmoja
tunaingiza umeme kwenye gridi ya taifa hatutasubiri kuwasha mitambo yote
minane.” Alisema Mhandisi Manda.
Alisema, mradi mzima ambao umeanza kutekelezwa rasmi Machi 3, 2016,
utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 344,059,746.00 kati ya hizo asilimia 15
zimetolewa na serikali.

“ Kufikia leo Juni 17, 2017, asilimia 63 ya ujenzi wa mitambo imekamilika, na tunahakika
ya kukamilisha ujenzi wa jumla kwa vile tayari mitambo yote inayohitajika
imeshalipiwa na mingine iko njiani inaletwa nchini.” Alifafanua na kuongeza
mitambo yote iliyoagizwa na TANESCO imo kwenye makontena 900 na tayari makontena 400 na ushee yamekwishawasili na baadhi ya mitambo imefungwa na
tunatarajia mashine zingine kwenye hayo makontena yaliyosalia zitawasili nchini
wakati wowote. Alisema.

Akizungumzia kuhusu makontena 20 yaliyokuwa yamezuiliwa na TRA bandarini, Mhandisi Manda
alisema, taarifa hizo hazina msingi wowote kwani kiasi hicho cha makontena 20
ni sehemu ya makontena 900 na tayari TANESCO imeshalipa fedha hizo za kodi na
mizigo hiyo imefika site.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Mwinuka;pia alitembelea
mradi wa umeme wa upanuzi wa Kinyerezi II ambako nako ameridhishwa na kasi ya
ujenzi wake.
 


Mradi huo ambao unasimamiwa na Mhandisi Simon Jilima, utawezesha ongezeko la megawati 35na hivyo Kinyerezin I ambayo inatoa Megawati 150 itakuwa na uwezo wa kutoa
Megawati 185 za umeme.


 Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda
 Meneja wa mradi wa upanuzi Kinyerezi I, Mhandisi Simon Jilima.
 DKT. Mwinuka, (kulia), Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (katikati) na Meenja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen A.S.Manda, wakijadiliana jambo.
 Mitambo ikiteremshwa eneo la ujenzi.
 Mkurugenzi wa Business Times, Imma Mbuguni (kulia) akizungumza jambo na Mhandisi, Khalid James
 Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere(kulia), akiteta jambo na Kaimu Meneja Uhisano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji
 Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O.Ikwasa (kulia), akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere.
 Mhariri Mtendaji wa Business Times, Bw. Imma Mbuguni, akizungumza ili kuoata ufafanuzi wa maswala kadhaa
 Baadhi ya mitambo ikiwa eneo la ujenzi ikisubiri kuunganishwa
 Mtandao wa nguzo za umeem ukiwa tayari kwa sehemu kubwa
 Kaimu Meenja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji akifafanua baadhi ya mambo kuhusu namna Shirika hilo linavyotekeleza sera ya kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility), ambapo alisema, licha ya shirika imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii sio tu kwenye maeneo ambako mradi unapita bali pia maeneo mengine na kutolea mfano wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, kamati ya kikosi kazi cha kuokoa mazingira, na hata shule. Kushoto ni Dkt. Mwinuka na Mhandisi Khalid James
 Dkt. Mwinuka akiwa amezungukwa na wasidizi wake akizungumza kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II
 Dkt. Mwinuka (kulia), akiongozana na wakandarasi toka kampuni ya kijapani SUMITOMO amabao ndio wanajenga mradi huo
Dkt. Mwinuka (kushoto), Mhandisi Ikwasa(katikati) na Mhandisi Chegere.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO DKT. TITO MWINUKA AWAHAKIKISHIA WATANZANIA MRADI WA UMEME WA GESI ASILIA WA KINYEREZI II UNAENDELEA KWA KASI
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO DKT. TITO MWINUKA AWAHAKIKISHIA WATANZANIA MRADI WA UMEME WA GESI ASILIA WA KINYEREZI II UNAENDELEA KWA KASI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzZSeMzU2zJ9YnCt3EH4BkmYEos4ZVmQHOJ1Dhw3k3zpYl14_iS6eN0TdKCBmBivVpWjR4KqAJqCas9E160S5wVQuHTJ9_HPbIBwtcvsOAEi3nB1BCucBU_00M-9mNq4z7tsBe-RGYXGY/s640/5R5A6030.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzZSeMzU2zJ9YnCt3EH4BkmYEos4ZVmQHOJ1Dhw3k3zpYl14_iS6eN0TdKCBmBivVpWjR4KqAJqCas9E160S5wVQuHTJ9_HPbIBwtcvsOAEi3nB1BCucBU_00M-9mNq4z7tsBe-RGYXGY/s72-c/5R5A6030.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kaimu-mkurugenzi-mtendaji-wa-tanesco.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kaimu-mkurugenzi-mtendaji-wa-tanesco.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy