KAIMU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGUA MKUTANO WA KAMATI NDOGO YA USALAMA WA RAIA YA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC)

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, akizungumza wakati wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa...


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, akizungumza wakati wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo  jijini Dar es Salaam. (PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

Mkurugenzi wa Masuala ya  Siasa,Ulinzi na Usalama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, akizungumza wakati wa  Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya hiyo, uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna  Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC), uliofanyika  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo  jijini Dar es Salaam.
Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Profesa Jean Kitembo Mbilika  ,akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),uliofanyika  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, leo  jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu kutoka Malawi, Michael Gama ,akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, leo  jijini Dar es Salaam.
 
Naibu  Mkuu wa Uhamiaji kutoka nchini Swaziland, Makhosi Simelane, akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo  jijini Dar es Salaam.
 
Naibu Balozi wa Zimbabwe nchini, Walter Sande akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),uliofanyika  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, leo  jijini Dar es Salaam.
 
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya (wa pili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Wa tatu kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo  jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, amewaomba washiriki wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuhakikisha wanapambana kupunguza vitendo vya ujangili, biashara ya magendo, biashara ya binadamu, uhamiaji haramu kwani vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi zilizopo katika jumuiya hiyo, hivyo kupelekea kurudi nyuma kwa shughuli za maendeleo na uchumi.
Balozi Simba aliyasema hayo alipozungumza katika Mkutano huo   uliojadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama katika maeneo ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo, uliohusu masuala ya uhamiaji, ukimbizi, mbuga na wanyamapori katika maeneo ya nchi wanachama wa jumuiya ya SADC, leo jijini Dar es Salaam.
“Hatuwezi kuendelea kiuchumi katika nchi zetu za wanachama wa   Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, kama matendo ya ujangili,biashara ya binadamu, masuala ya wakimbizi, uhamiaji haramu hayajatafutiwa ufumbuzi, kwani  haya yatazorotesha shughuli za kiuchumi ikiwepo utalii, hivyo ni bora tukayafanyia kazi maeneo hayo,” alisema Balozi Simba
Akizungumza wakati wa uchangiaji mada katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Masuala ya   Siasa, Ulinzi na Usalama wa   Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, alisema uhalifu katika mipaka ya nchi wanachama ikiwemo uwindaji haramu wa pembe za ndovu, uhamiaji haramu,biashara ya binadamu na madawa ya kulevya lazima vidhibitiwe kwani vikiachwa mbeleni  vitahatarisha Amani na utulivu uliopo katika nchi wanachama.
“Amani na utulivu katika nchi wanachama ni kichocheo cha mabadiliko ili kupiga hatua za kimaendeleo kwenda mbele na kushirikiana kukuza uchumi katika nchi wanachama wa SADC, hivyo yatupasa wote kwa pamoja kuunga mkono harakati za kukomesha vitendo vya uhalifu katika nchi na mipaka yetu,” alisema Cardoso
Aidha   washiriki wa mkutano huo kutoka katika nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Swaziland, Malawi, Zimbabwe kwa pamoja walikubaliana kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama katika nchi zao kudhibiti matendo yote yanayohatarisha amani na utulivu.
 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAIMU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGUA MKUTANO WA KAMATI NDOGO YA USALAMA WA RAIA YA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC)
KAIMU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGUA MKUTANO WA KAMATI NDOGO YA USALAMA WA RAIA YA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkO7iP5v0esbUvw3l-Xv8_Qb3C_0n_Mmsfw025cgwhaeUIuScNq6lKLQ8v58rqzkeLZ9dvETGZmKu6M1wR1nmqrLiwLtN4JeJfCMTOgkC2RiFFAB8SwJtgOQ50JiJjriEvpulicDh7V0g/s640/PIX+3..JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkO7iP5v0esbUvw3l-Xv8_Qb3C_0n_Mmsfw025cgwhaeUIuScNq6lKLQ8v58rqzkeLZ9dvETGZmKu6M1wR1nmqrLiwLtN4JeJfCMTOgkC2RiFFAB8SwJtgOQ50JiJjriEvpulicDh7V0g/s72-c/PIX+3..JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kaimu-katibu-mkuu-mambo-ya-ndani.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/kaimu-katibu-mkuu-mambo-ya-ndani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy