F JUMAA KAREEM KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA | RobertOkanda

Friday, June 16, 2017

JUMAA KAREEM KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amekutana na Masheikh na Viongozi wa Misikitini zaidi ya Mia sita (600) ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Hatua hii ni mwendelezo wa Mikutano yake na Makundi ya watu mbalimbali, ambapo katika kuenzi mwezi wa Mfungo wa Ramadhani.

Mhe Makonda ametoa vitu mbalimbali kama Sadaka kwa kila kiongozi kwa kila Sheikh wa Mkoa wa Dar eas Salaam:-
1. Mchele Kg 25
2. Ngano Kg 25
3. Sukari Kg 25
4. Mafuta ya kupikia Lita 20

Akizungumza na Masheikh na  Viongozi wa Dini ya Kiislamu, Mhe Makonda amewapongeza kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali pamoja na kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi ambavyo anatekeleza majukumu yake ya kazi kwa kuhakikisha anaifanya Tanzania kuwa Nchi ya Uchumi wa kipato cha kati na mapinduzi ya Viwanda.

Mhe Makonda pia, amewaomba viongozi wa Dini kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kuhubiri Amani, Utulivu na Uvumilivu katika mambo waumini wao wanayofanya.

Katika hatua nyingine, Mhe Makonda amefanikiwa kuwashawishi wafanyabiashara hasa wa Supermarket kwa Mkoa wa Dar es Salaam kufanya kazi mpaka saa sita za usiku, ili kutoa fursa kwa wananchi kujipatia mahitaji yao muhimu kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Kitengo cha Mawasiliano
16/06/2017

0 comments:

Post a Comment