JUMA NATURE, KHADIJA KOPA, NA TWANGA PEPETA WATUMBUIZA MKESHA WA MWENGE WA UHURU VIWANJA VYA BARAFU MANISPAA YA UBUNGO

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania akiwemo msanii mkongwe katika soko la muziki Juma Kasim...



Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania akiwemo msanii mkongwe katika soko la muziki Juma Kasim maarufu kama Juma Nature, Msanii mkongwe wa Muziki wa taarabu Khadija Omar Abdallah Kopa maarufu kama Malkia wa Mipasho, Band ya Twanga Pepeta sambamba na wasanii wengine zaidi ya kumi wametumbuiza kwenye sherehe za Mkesha Wa Mwenge wa Uhuru 2017 zilizofanyika usiku wa kuamkia Leo Tarehe 1, Juni 2017 katika Viwanja Vya Barafu, Manispaaya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Katika Sheree hizo zilizoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kwa ushirikiano Mkubwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo sambamba na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wananchi waliitikia wito kwa kujitokeza kwa wingi Jambo ambalo limeimarisha umahiri wa Mwenge wa Uhuru ambao kwa mwaka huu una kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu.
Pamoja na kauli mbiu ya kutilia msisitizo kuhusu uchumi was viwanda pia Mwenge was Uhuru umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria sambamba na kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Awali kabla ya mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Viwanja hivyo vya Barafu-Mburahati Mwenge huo ulizuru katika miradi mitano katika Manispaa hiyo Kama ifuatavyo;
1. Uzinduzi wa Jengo la Kituo Cha Huduma kwa wagonjwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) katika kituo Cha afya Mbezi. Jengo hilo limegharimu kiasi cha Tshs 125 milioni  ambazo zimetolewa na wafadhili ambao ni MDH (Management and Development for Health).
2. Kuweka Jiwe la Msingi wa Kituo Cha Polisi Cha Kati-Kata ya Kibamba ambapo wananchi wamekwisha changia jumla ya Tsh. 53,000,000/ = huku NSSF ikichangia Tsh. 50,000,000/= sawa na jumla ya Tsh. 103,000,000/=
3. Uzinduzi wa madarasa nane katika Shule ya Msingi Malambamawili Kata ya Msigani, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam. Jengo hilo lenye madarasa nane (8) yaliyozinduliwa yamejengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu kwa  gharama ya Shilingi Milioni mia moja na thelethini na sita (Tshs 136,000,000/=)., madarasa hayo Yakikamilika shule itakuwa na vyumba vya madarasa 24.
4. Uzinduzi wa Mradi wa Mabasi SIMU 2000 Uliopo katika Kata ya Sinza. Kituo hicho kimejengwa kwa kutumia fedha zilizotokana na Mapato ya Ndani (Own Source)  Gharama yake ni Shilingi 2,376,647,991.89 chini ya Mkandarasi M/S DEL MONTE (T) LTD.
5. Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Mburahati katika eneo la Mtaa wa NHC Kata ya Mburahati. Mradi huu wa ujenzi wa zahanati  ulianza kutekelezwa tangu Juni 2014 na kukamilika mnamo Oktoba 2016 chini ya Manispaa ya Ubungo, kwa gharama ya kiasi cha Tshs 84,000,000.00.
Tayari Mwenge wa Uhuru umekwisha ondoka Katika Mkoa wa Dar es sala ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.
Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JUMA NATURE, KHADIJA KOPA, NA TWANGA PEPETA WATUMBUIZA MKESHA WA MWENGE WA UHURU VIWANJA VYA BARAFU MANISPAA YA UBUNGO
JUMA NATURE, KHADIJA KOPA, NA TWANGA PEPETA WATUMBUIZA MKESHA WA MWENGE WA UHURU VIWANJA VYA BARAFU MANISPAA YA UBUNGO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEio4wqU3kB2tgbR0pESxX4SzaFBNJCH5bWXYGjG_-4VCuDogthw539UxDYFaEcKdRv-ovrsHyj9a4CCzTjgCZ8WCbDXK9D-nZ60QCvRnAf11BMv9Ava68Do3pTfl_GPEf4VTprtSqSnyf0K/s640/FB_IMG_1496333182265.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEio4wqU3kB2tgbR0pESxX4SzaFBNJCH5bWXYGjG_-4VCuDogthw539UxDYFaEcKdRv-ovrsHyj9a4CCzTjgCZ8WCbDXK9D-nZ60QCvRnAf11BMv9Ava68Do3pTfl_GPEf4VTprtSqSnyf0K/s72-c/FB_IMG_1496333182265.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/juma-nature-khadija-kopa-na-twanga.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/juma-nature-khadija-kopa-na-twanga.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy