Afisa Utumishi Mkuu Ally Juma Ally (Kushoto) akisikiliza maswali mbalimbali ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakati wa kikao cha ...
Afisa
Utumishi Mkuu Ally Juma Ally (Kushoto) akisikiliza maswali mbalimbali
ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakati wa kikao cha Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Yamo Wambura
Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Mariam Maliwa akifatilia kwa karibu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Mariam Maliwa akifatilia kwa karibu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo Ndg Alute Joseph akitoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma
Leo
June 20, 2017 watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameanza
kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano mkubwa
uliohudhuriwa na watumishi wote wa makao makuu katika ukumbi wa Manispaa
hiyo mkutano ambao umeongozwa na Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa hiyo
Ndg Ally Juma Ally kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo.
Akiongea
katika kikao hicho mara baada ya kufungua kikao Afisa Utumishi mkuu
aliwajulisha kuanza rasmi kwa wiki ya utumishi na kutoa utaratibu wa
jinsi Halmashauri itakavyotimiza maadhimisho hayo ambapo alisema kuwa
kwa wiki hii ya maadhimisho muda wa kutoka kazini utaongezeka kwa saa
moja badala ya kutoka saa tisa na nusu mchana itakuwa ni saa kumi na
nusu, hali kadhalika alisisitiza mambo ya kuzingatia katika wiki hii na
hata baada ya maadhimisho no pamoja na Kufanya kazi kwa kuzingatia
sheria,kanuni taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma,
Kufanya kazi zetu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, na Kufanya
kazi kwa uadilifu mkubwa bila ya viashiria vya kupokea rushwa au hongo
katika kutoa huduma katika ofisi za serikali au umma.
Mengine
ni Kuongeza Ari na kujituma katika kutekeleza majukumu yetu, Kufanya
kazi kwa maarifa na kuwasikiliza wanaanchi wanapofika kupata huduma
katika ofisi za umma/serikali na Kuweka vizuri kumbukumbu za wananchi
watakaohudumiwa kwa kipindi hiki ili kuzitolea taarifa kwenye mamlaka
husika.
Pia
wamesisitizwa kutoa Huduma bora, Utii kwa serikali, Kuongeza bidii ya
kazi, Kutoa huduma bila upendeleo, Kufanya kazi kwa Uadilifu,
Uwajibikaji kwa Umma, Kuheshimu sheria na taratibu za kazi, na Matumizi
sahihi ya Taarifa.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
COMMENTS