ESRF YATOA MAFUNZ YA UANDAAJI WA MIPANGO MIKAKATI KWA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MIKOA NA WILAYA

Hapa chini Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imetoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugen...

Hapa chini Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imetoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati ambayo itatumika katika halmashauri za mikoa hiyo. Akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi hao kwani yatawasaidia kupata mbinu mpya ambazo watazitumia wakati wa kutengeneza mipango mikakati katika maeneo yao. Alisema kwa dhamana waliyonayo watumishi hao ni vyema kutumia mafunzo hayo ya siku mbili vizuri ili baada ya mafunzo waweze kupata njia mbadala katika uandaaji wa mipango mikakati ambayo itasaidia kuleta maendeleo.
 
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati[/caption] “Hampo hapa kwa ajali, mpo kwasababu dhamana zenu ni kubwa, kwa kupitia mafunzo haya mtapata nyezo za kupangia mikakati ya kweli na mimi nataraji mtatoka hapa vizuri, haya ni mafunzo muhimu sana, “Tusiishie kwenye mikakati, tatizo ni jinsi gani ya kuanzisha miradi, tumekuwa na mawazo mengi sana lakini tuna changamoto ya kuyaweka kwenye miradi, tutoke kwenye kuwa na mawazo na sasa tuanze kuyafanyia kazi,” alisema Mongela. Pia Mongela aliwashukuru ESRF kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwataka washiriki kufanya kazi kwa ushirikiano na ESRF kwani tayari wameonyesha nia ya kushirikiana nao ili kuhakikisha mipango ambayo wanaipanga inafanyiwa kazi. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwenye mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati.[/caption] “Tuone jinsi gani tunatumia fursa hii vizuri, tunatakiwa tukitoka hapa tukatekeleze mipango hii na ESRF wapo tayari kushikana mikono na sisi hadi waoane mafanikio na mimi niwahakikishie sisi tupo tayari … nategemea mambo makubwa baada ya kuanzisha ushirikiano huu,” alisema Mheshimiwa Mongela. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa mstali wa mbele kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa muhimu kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. “Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wa nje na ndani ya nchi, ESRF imekuwa ikisimamia na kuhimiza ufikiwaji wa malengo hayo sio tu katika ngazi ya Taifa bali pia katika ngazi ya wilaya na hata Kata,” alisema Dk. Kida.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: ESRF YATOA MAFUNZ YA UANDAAJI WA MIPANGO MIKAKATI KWA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MIKOA NA WILAYA
ESRF YATOA MAFUNZ YA UANDAAJI WA MIPANGO MIKAKATI KWA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MIKOA NA WILAYA
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/06/2.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/esrf-yatoa-mafunz-ya-uandaaji-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/esrf-yatoa-mafunz-ya-uandaaji-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy