DG WA PPF WILLIAM ERIO AUNGANA NA WAFANYAKAZI KUHUDUMIA WAWANACHAMA WA MFUKO, KATIKA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA

  Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (kushoto), akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, Clemence Munisi, aliyefika kitengo...



 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (kushoto), akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, Clemence Munisi, aliyefika kitengo cha huduma kwa wateja ili kuhudumiwa wakati wa kilele cha wiki ya utumishi Makao Makuu ya PPF Barabara za Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam, Ijumaa Juni 23, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAKATI siku ya Wiki ya Utumishi wa Umma imefikia kilele leo Juni 23, 2017, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, alijiunga na kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Mfuko huo Makao Makuu ya PPF barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam na kuwahudumia wateja.
Awali Bw. Erio alizungumza na baadhi ya wanachama wa Mfuko waliofika kwenye kitengo hicho kuhudumiwa na kusikiliza maoni yao ni jinsi gani wanahudumiwa na Wafanyakazi wa Kitengo hicho.
Aidha Bwana Erio pia aliwahudumia wanachama wengine akiwemo mzee Clemence Munisi ambaye ni mstaafu wa kampuni ya Narco.
Kwa mujibu wa Mzee Munisi, yeye alisema, amefurahishwa na huduma zitolewazo na Mfuko ambapo zimekuwa ni za haraka na zisizokuwa na usumbufu.
Baada ya kutembelea kitengo hicho, pia alikutana na baadhi ya wafanyakazi ili kusikiliza maoni yao kuhusu namna uongozi wa Mfuko unavyoshirikiana na wafanyakazi katika kulihudumia taifa.
“Kama mjuavyo hii ni siku ya mwisho ya wiki ya utumishi, nimeona nikutane nanyi ili kuwasikiliza, maana mara nyingi sisi viongozi ndio tunasema tu, lakini leo ni zamu yenu ninyi watumishi kusema jambo lolote linalohusu Shirika letu, lakini hata wewe binafsi kama mfanyakazi.” Alisema Bw. Erio.
 Pia aliwakumbusha wafanyakazi kuwajibika ipasavyo katika kuwahudumia wananchi, lakini pia kuzingatia suala la afya bora.
“ Ili uweze kuwahudumia vema wananchi, ni lazima uwe na afya bora, mimi kama mwenyekiti wa kamati ya UKIMWI ya shirika letu, bado nasisitiza, chukueni tahadhari kubwa, kwani ugonjwa huu bado upo ingawa hauzungumzwi sana kwa sasa.” Alionya Bw. Erio.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa wafanyakazi hao kutojihusisha kwa namna yoyote na matumizi ya madawa ya kulevya au biashara ya madawa ya kulevya.
Mimi siko serikalini, lakini ninao wajibu kama kiongozi wenu, kuwakumbusha mambo ambayo jamii inapaswa kujiepusha nayo, na nyinyi kama sehemu ya jamii, hamna budi kutojihusisha kwa namna yoyote na matumizi au biashara ya madawa ya kulevya.” Alisema.
Kwa upande wao wafanyakazi walishukuru uongozi wa Mfuko kwa kuwa karibu na wafanyakazi.
“Ukiona hupati maneno mengi ujue mambo yako poa, sisi kwa kweli tunashukuru sana kwa kiongozi kama wewe kuja kuzungumza nasi tena kwa kutusikilzia sisi tuna lipi la kusema, lakini nikuhakikishie tu kwa niaba ya vijana wenzangu, mimi naona mambo yako safi na sikukuu hii tutasherehekea kwa furaha kabisa.” Alisema mfanyakazi mmoja kutoka idara ya fedha, Bwana Joseph Fungo.
Naye Meneja wa fedha wa PPF, Dozitte Msoffe, alisema mahusiano mema kati ya uongozi na wafanyakazi ndiyo yanayoboresha utoaji huduma kwa wananchi na kwa PPF, kumekuwepo na mahusiano mazuri sana baina ya pande hizi mbili kwa hivyo mimi nikupongeze tu ndugu Mkurugenzi Mkuu, kwa uamuzi wako wa kuja kutusikiliza hii huwezi kuisikia mahala pengine, lakini hapa PPF imetokea hongera sana.” Alisema Bw. Msoffe.

 Bw. Erio akizungumza na baadhi ya wanachama waliofika kitengo cha huduma kwa wateja cha Mfuko huo ili kupaiwa huduma
 Meneja wa Fedha wa PPF, Dozitte Msoffe akizungumza. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
 
 Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Bw. Erio
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko huo Makao Makuu, PPF House, barabara ya Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam, Ijumaa Juni 23, 2017 wakati wa kilele cha wiki ya utumishi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mfuko huo, Bi.Gladness Mteta, na kulia ni Kaimu Katibu M,uu wa TUICO, Bw.Laurent Mwombeki.
 Bw. Msoffe akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio na watumishi wengine wakimsikilizia
 Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Bw. Erio kwa makini
 Afisa Fedha wa PPF, Bw. Joseph Fungo akizungumza
 Baadhi ya wafanyakazi wakipiga makofi kufuatia mazungumzo mafupi ya Bw. Erio
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Gladness Mteta, (kulia) akiwa na Meneja wa Huduma za Utawala wa PPF, Cecilia Obeid Katikaza.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DG WA PPF WILLIAM ERIO AUNGANA NA WAFANYAKAZI KUHUDUMIA WAWANACHAMA WA MFUKO, KATIKA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA
DG WA PPF WILLIAM ERIO AUNGANA NA WAFANYAKAZI KUHUDUMIA WAWANACHAMA WA MFUKO, KATIKA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgF5meXQf3UIex4a9x_yLMN-7_NkzRFx0lRsYgXjx7qutFx49JoRTaq6lXyOnWchZA48k9mE4dycfoXO_1GAyfkdInXtMisFnsfv4TiIR5eSa9daq4d60uPkw9efGV6qTNCPK9ofe8Vw1k/s640/5R5A7537.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgF5meXQf3UIex4a9x_yLMN-7_NkzRFx0lRsYgXjx7qutFx49JoRTaq6lXyOnWchZA48k9mE4dycfoXO_1GAyfkdInXtMisFnsfv4TiIR5eSa9daq4d60uPkw9efGV6qTNCPK9ofe8Vw1k/s72-c/5R5A7537.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/dg-wa-ppf-william-erio-aungana-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/dg-wa-ppf-william-erio-aungana-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy