DC KASESELA TUTAUFUNGA MGODI WA NYAKAVANGALA HALI IKIENDELEA HIVI

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na blog hii juu ya kitu kinachiendelea kwenye mgodi wa nyakavangala. N...


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na blog hii juu ya kitu kinachiendelea kwenye mgodi wa nyakavangala.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wachimbaji wa madini katika mgodi wa nyakavangala wamefukiwa na mchanga kutokana na wachimbaji hao kuingia kinyume cha makubaliano yaliyowekwa baina ya wachimbaji na Mkuu wa Wilaya ya Iringa  Richard Kasesela.

Akizungumza na blog hii Kasesela alisema kuwa Jana mida ya saa 1 jioni Duara la mgodi mmoja ulioko Nyakavangala uliporomoka na kufukia wachimbaji 4 . 

"Inasemekana wachimbaji hao walikuwa wameingia kuiba kwani duara hilo ni kati ya maduara ambayo Mkuu Wa wilaya ya Iringa  Mhe Richard Kasesela aliifungia ili ijengwe nguzo na ngao" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa Watu 4 waliingia mgodini baada ya mafundi  Wa ujenzi Wa ngao kupumzika kwa vile ni usiku ndipo wachimbaji nao wakaingia mgodini bila ruhusa

"Hadi sasa tumefanikiwa kuokoa 3 mpaka sasa huyo mmoja hajaokolewa bado yupo ndani ya mgodi kutokana na changamoto za uokoaji ili Juhudi zinaendelea za kumuokoa huyo mmoja" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa changamoto ilikuwa ni namna ya kumuokoa kwani sehemu iliyokuwa imejifukia juu mwamba mwingine ulionekana kuwa na dalili za kushuka.ikawapasa kujengea kwanza eneo hilo kazi iliyochukua mda mrefu na ndipo waaze kuokoa.kwahiyo tunasubiri hatua nyingine sasa.

"Naendelea kuwaonya wachimbaji wasiendelee na uchimbaji eneo la chini maarufu kama kwenye "vein" mpaka wajenge ngao ili wasihatarishe maisha yao. Wakiendelea na kiburi tutaamua tufunge mgodi" alisema Kasesela

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DC KASESELA TUTAUFUNGA MGODI WA NYAKAVANGALA HALI IKIENDELEA HIVI
DC KASESELA TUTAUFUNGA MGODI WA NYAKAVANGALA HALI IKIENDELEA HIVI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2a_cl7FQwLNBHUmSYpZdlj02-4IWN9U5Eb4GcE5sXL-ueBv80nxtmybjmWBnnZ07yiXYkvXNyXbcRja94oBWVRkCSc42_IXYZCILbZO37JdB2gNjmJIhSQYQ-IQfv3BHLDyh2vNpsNXvc/s640/IMG-20170610-WA0139.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2a_cl7FQwLNBHUmSYpZdlj02-4IWN9U5Eb4GcE5sXL-ueBv80nxtmybjmWBnnZ07yiXYkvXNyXbcRja94oBWVRkCSc42_IXYZCILbZO37JdB2gNjmJIhSQYQ-IQfv3BHLDyh2vNpsNXvc/s72-c/IMG-20170610-WA0139.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/dc-kasesela-tutaufunga-mgodi-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/dc-kasesela-tutaufunga-mgodi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy