BENKI YA FINCA, DAR CITY F.C ZA SAINI MKATABA WA UDHAMINI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Meneja Masoko wa Benki ya FINCA, Nicholous John, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kus...


Meneja Masoko wa Benki ya FINCA, Nicholous John, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 na Klabu ya soka ya Dar City FC. Kulia ni Rais wa Klabu hiyo, Azimkhan Akber Azimkhan na Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo

Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo akizungumza katika mkutano huo.

Wakihakiki mkataba hiyo wakati wa kutiliana saini.


Waandishi wa habari wakichukia taarifa za tukio hilo.



Hapa mkataba ukiangaliwa baada ya kusainiwa.

Meneja Masoko wa Benki ya FINCA, Nicholous John (kushoto), akikabidhi jezi kwa Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo (wa pili kulia) na Makamu wa Rais wa Dar City Club, Hamidu Zuberi.


Makabidhiano tena.

Na Dotto Mwaibale

Benki ya FINCA Microfinance leo imesaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 na klabu ya soka ya Dar City FC.
Mkataba huo uliosainiwa jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya Benki ya FINCA , makubaliano hayo yanajumuisha kuipatia jezi za michezo klabu hiyo pamoja na kuipatia timu fedha za usafiri na mahitaji mengine ya msingi katika msimu ujao wa ligi Daraja la Pili.

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano Meneja amasoko wa FIINCA, Nicholous John alisema kwamba udhamini huo ni kuthibitisha tena sera ya benki hiyo ya kujikita katika kusaidia wajasiriamali vijana, kuhakikisha wanakua na waje kuwa watu waliofanikiwa katika sekta ya kifedha na hali kadhalika katika jamii kwa ujumla.

“FINCA tunaamini katika kukuza umuhimu wa kukuza uchumi ndani ya jamii, hususani vijana, na ndio maana tulikuwa tayari kukubaliana na juhudi za ziada za vijana hawa baada ya kubaini kwamba wanavyo vipaji vya kuwawezesha kufika mbali kulingana na hali ya michezo ilivyo,” alisema John na kuongeza kwamba wameamua kujumuisha utamaduni wa ujasiriamali katika michezo.

Dar City FC ambayo ilifanikiwa kuingia katika mashindano ya Kombe la Mabingwa wa shirikisho hivi karibuni inatarakiwa kusafiri hadi Kahama, mkoani Shinyanga ambako itaungana na timu nyingine saba katika ligi ya mabingwa wa mikoa nchini.
Aidha Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan aliishukuru FINCA kwa ukarimu huo wa msaada akisema kuwa umekuja wakati sahihi na katika kipindi ambacho klabu hiyo inakabiliwa na changamoto za kifedha.

“Tunatoa shukrani nyingi kwa Benki ya FINCA kwa msaada huu uliokuja kwa wakati mwafaka, sasa hivi tuna uhakika kwamba tutafanya vizuri katika mashindano kwa kuwa udhamini huu utatuwezesha kwa kiwango kikubwa kwa timu kuwa na morali na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii, “ alisema Azimkhan.

Alifafanua kuwa matayarisho kwa ajili ya mashindano hayo yanajumuisha mahitaji kadhaa na hiyo ni changamoto kwa makampuni mengine, watu binafsi na mashirika katika kuzisaidia timu zinazoibua kwa kutambua umuhimu wake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo wakati akiishukuru FINCA kwa udhamini wake alitoa wito kwa taasisi nyingine za kifedha kuiga mfano maridhawa wa FINCA kwa kuzisaidia klabu nyingine za soka zinazoibukia ndani ya jiji.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BENKI YA FINCA, DAR CITY F.C ZA SAINI MKATABA WA UDHAMINI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
BENKI YA FINCA, DAR CITY F.C ZA SAINI MKATABA WA UDHAMINI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjf8ObJ19klqVu4UhM5YNO_IFrY9u-sp5Abf3rIpgHEe89vBanwHE4v5TwWM2_JehouFT10HsdDj3RysAuIWUDIUAfdXPoHURA8QfU2PoD_I5PtwaJ_YnnMg1TFBFhA62sPRi0tjRuGdyvA/s640/IMG_8754.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjf8ObJ19klqVu4UhM5YNO_IFrY9u-sp5Abf3rIpgHEe89vBanwHE4v5TwWM2_JehouFT10HsdDj3RysAuIWUDIUAfdXPoHURA8QfU2PoD_I5PtwaJ_YnnMg1TFBFhA62sPRi0tjRuGdyvA/s72-c/IMG_8754.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/benki-ya-finca-dar-city-fc-za-saini.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/benki-ya-finca-dar-city-fc-za-saini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy