F AIRTEL NA VETA WATANGAZO KOZI TANO MPYA KUSOMWA KWA NJIA YA SIMU YA MKONONI | RobertOkanda

Wednesday, June 14, 2017

AIRTEL NA VETA WATANGAZO KOZI TANO MPYA KUSOMWA KWA NJIA YA SIMU YA MKONONIKaimu Mkurugenzi mkuu wa VETA nchini ,Bwire Ndazi akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu mpya ya mafunzo ya ufundi stadi kupita mtandao wa airtel kwa watu waliopo mbali na vyuo inayokwenda kwa jina la VSOMO
 Mkurugezni wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania ,Betrice Singano  akizungumza na waandishi wa habaari waati wa uzinduzi wa programu ya VSOMO inayoendeshwa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ufundi Stadi nchini VETA
Mkurugezni wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania ,Betrice Singano  akizungumza na waandishi wa habaari waati wa uzinduzi wa programu ya VSOMO inayoendeshwa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ufundi Stadi nchini VETA
 Kaimu Mkurugenzi mkuu wa VETA nchini ,Bwire Ndazi  Akionyesha Application iliyopo kwenye simu ya Airtel ambayo itasaidia mtu anayyetumia mtandao huo kujiunga na mafunzo y ufundi Stadi Popote pale alipo kushoto ni Mkurugezni wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania ,Betrice Singano na  kulia ni Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Habibu Burko  akishuhudia
 Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa ,Mhandisi Luuciius ,luteganya akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya VSOMO Katika chuo cha VETA Kipawa.
 Sehemu ya wanafunzi wa chuo cha VETA kipawa walio shuhudia tukio hilo la uzinduzi
Picha ya pamoja kati ya watendaji wa VETA,AIRTEL na Wanafunzi mara baada ya kumalizika kwa uzinduuzi wa programu ya VSOMO

Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania imeboresha huduma yake ya kutoa elimu kwa njia ya mtandao inayokwenda kwa jina la VSOMO kwa kushirikiana na mamlaka ya ufundi stadi nchini VETA kupitia chuo cha Kipawa.

Akizungumza wakati wa kutangaza uongezwaji wa programu zingine 5 na kufanya kozi zinazofundishwa kuwa 11 Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania , Beatrice Singano amesema mpango huo ni sehemu ya programu ya  Airtel Fursa inayoendeshwa na kampuni hiyo.

“Airtel fursa imeendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuelekea Tanzania ya Viwanda kwa kuwawezesha watanzania kupata elimu ya ufundi stadi popote pale walipo ili waweze kuajiriwa au kujiajiri katika mashirika mabalimbali”alisema Singano.

Ametaja kuwa Airtel Tanzania iimefaanya tafiti na kubaini kuwa vijaana wengi wamekuwa waoga wa kujiunga na shule au kujiendeleza katika ufundi stadi kwa hofu ya kupoteza wateja wao katika biashara wanazofanya pindi wanapokwenda shule kutwa nzima.

Amesema kuwa mpango huu wa elimu kwa njia ya mtandao ni moja ya fursa ambayo itasaidia vijana wengi hivyo mtu anaehitaji kupata mpango huu anatakiwa kujiunga na Airtel Tanzania hili aweze kunufaika na mpango huu.

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Veta,Bwire Ndazi ametaja kuwa mpango huu ni muhimu sasa kwani utawezesha VETA kufikia malengo yake iliyojiwekea ya kutoa elimu ya ufundi mpaka vijijini hili kuwawezesha watanzania kupata elimu pale walipo.

Ametoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Airtel fursa kwa kuwezesha tasisi za elimu kutoa mafunzo kwa njia ya kisasa zaidi.

0 comments:

Post a Comment